
Kiungo mwalimu: Kiwango alichoonesha Sami Khedira katika fainali za mwaka 2014 za kombe la dunia kimewavutia wengi.
ASERNAL wamejiandaa kuwapiga bao Chelsea kwa kumsajili kiungo wa Ujerumani, Sami Khedira kutoka klabu ya Real Madrid.
Magazeti ya Hispania yunaripoti kuwa dili hilo la paundi milioni 23 limeshakubaliwa.
Kwa mujibu wa Sport, Khedira atasaini mkataba wa miaka minne katika dimba la Emirates, licha ya Chelsea kujitokeza kuitaka saini ya mtaalamu huyo.
Mazungumzo
ya mkataba mpya baina ya wawakilishi wa nyota huyo mwenye miaka 27 na
Real Madrid yalivunjika, hivyo kilichobaki ni kumuuza majira haya ya
kiangazi.


Amezama kwenye busu: Khedira akishangilia ubingwa wa Ujerumani katika dimba la Maracana.

Kwenye rada: Khedira alifunga bao katika mechi ya nusu fainali baina ya Ujerumani dhidi ya Brazil
Tayari
Asernal wameshatumia paundi milioni 30 kumnunua mshambuliaji wa Chile,
Alexis Sanchez kutokea klabu ya Barcelona, na wamefanikiwa kumsajili
beki wa kulia wa Ufaransa katika fainali za kombe la dunia, Mathieu
Debuchy kutoka klabu ya Newcastle.
Kocha
wa Chelsea, Jose Mourinho, aliyefanya kazi na Khedira wakati akiwa
Real Marid yuko makini kumsajili kiungo huyo wa ulinzi, lakini
anaonekana atamkosa.
Khedira alikosa mechi ya fainali jana jumapili baada ya kupata majeraha wakati akiwa mazoezini.
Hata
hivyo, alijumuika na wenzaka katika sherehe za ubingwa baada ya
Ujerumani kuipiga Argentina bao 1-0 na kutwaa kombe la dunia mwaka 2014
nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment