Muigizaji mwanamke nchini Marekani aliyemtumia Rais Barack Obama barua iliyokuwa na sumu ya Ricin amefungwa jela kwa miaka 18. Shannon Richardson, mwenye umri wa miaka 36,
kutoka Texas, pia alimtumia meya wa New York Michael Bloomburg barua
nyingine iliyokuwa na sumu hiyo hiyo.
Shannon Richardson ameigiza katika vipindi vya 'The Vampire Diaries' na 'The Walking Dead.
Shannon mwenye watoto sita aliomba mahakama kumhurumia kwa kumpa adhabu ndogo
Kulingana na viongozi wa mashitaka, moja ya
barua alizomtumia Obama , ilikuwa na maandihsi haya: "kilicho ndani ya
barua hii, hakiwezi kulinganishwa na mipango yangu kwako bwana Rais. ''
Barua nyingine iliyopokewa na meya Bloomberg,
anayeunga mkono kudhibitiwa kwa bunduki, ilisema, '' mpige risasi mtu
yeyote atayekuja kuchukua bunduki za mtu aliyetuma barua hii.''
Barua ya tatu iliyokuwa na kemikali hiyo ya
sumu, ilifunguliwa na bwana Mark Glaze, mkurugenzi mkuu wa idara
inayofadhiliwa na Meya ya kupambana na silaha haramu.
Richardson katika kumtaka jaji kumhurumia, aliomba
msamaha akisema, '' mimi sio mtu mbaya. Sina nia ya kumdhuru mtu yeyote.
Aliomba msamaha na huruma na kusema tayari anahisi
ameadhibiwa vya kutosha kwa kunyang'anywa watoto wake sita.
0 comments:
Post a Comment