Mdomo Wamponza Kafulila.....IPTLYamdai fidia ya sh. Bilioni

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL),
imemfungulia kesi Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
(NCCR-Mageuzi) katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ikimtaka
aombe radhi na kulipa fidia ya Sh bilioni 310.Katika kesi hiyo ya
madai, Kafulila anadaiwa kuidhalilisha kampuni hiyo, kutokana na kauli
alizotoa dhidi yake (IPTL).IPTL na walalamikaji wengine Pan Africa
Power Solution (PAP) na Mkurugenzi wa PAP, Harbinger
Sethwanamlalamikia Kafulila kuwatuhumu kuchukua fedha kinyume cha
sheria katika akaunti ya Escrow iliyopo Benki Kuu ya Tanzania
(BoT).Walalamikaji hao kupitia kwa Wakiliwao, Augustine Kusalika
wamefungua kesi hiyo, wakitaka Kafulila awalipe Sh bilioni 210
kamafidia ya kutoa kauli za udhalilishaji, kuwasababishia hasara
katika biashara na kuharibu mtazamo wa biashara zao.Aidha, wanaiomba
Mahakama iamuru Kafulila, awaombe radhi, piaawalipe Sh bilioni 100
kama hasara ya jumla pamoja na usumbufu walioupata, kutokana na kauli
za udhalilishaji.Kwa mujibu wa hati ya madai, iliyopatikana mwishoni
mwa wiki, Juni mwaka huu Kafulila alitangazakuwa IPTL na Seth,
walijipatia fedha kutoka akaunti ya Escrow kinyume cha sheria na
kumuita Seth ni 'Singasinga', jambo lililomdhalilisha na kumharibia
muonekano wake na biashara yake.Walalamikaji hao wanadai kupitia
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, bila kuwa na haki, Kafulila
alitoa taarifa hizo, kuwa IPTL inajihusisha na biashara zisizo halali
na za uongo, jambo lililosababisha jamii kuamini na kuwaharibia
mtazamo wa kibiashara.Aidha, wanadai Kafulila akiwa mbunge alipoteza
kinga ya wabunge inayowalinda wakizungumza bungeni, kwa kuwa alitoa
taarifa hizo nje ya shughuli zaBunge.Walidai Kafulila anaendelea
kutoka taarifa hizo, licha ya kumpa taarifa kwa maneno na maandishi,
wakimtaka kuacha kufanya hivyo, kwa kuwa anawaharibia biashara kitaifa
na kimataifa.Kwa mujibu wa hati ya madai, IPTL iliingia mkataba na
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kusambaza umeme
kwenye shirika hilo, lakini kulitokea mgogoro kati ya IPTL, Kampuni ya
VIP Engineering and Marketing na Tanesco, jambo lililosababisha wafike
Mahakama Kuu.Kutokana na mgogoro huo, Mahakama iliamuru Sh bilioni 200
zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow, zisitolewe hadi kesi hiyo
itakapokwisha na baada ya kesi kuisha, Mahakama iliamuru IPTL ichukue
fedha hizo.Walalamikaji hao wanadai licha ya Kafulila, kujua kuwepo
kwa mgogoro huo, aliendelea kutoa tuhuma hizo, huku akijua kuwa IPTL
imechukua fedha hizo kwa amri halali ya Mahakama.Wakili huyo alisema
wateja wake, wanaiomba Mahakama iamuru Kafulila awalipe Sh bilioni 310
kamafidia, aombe radhi, alipe gharama za uendeshaji wa kesi hiyo na
amri nyingine, ambazo Mahakama itaona zinafaa. 

0 comments:

Post a Comment