Ofisi
ya Ustawi wa Jamii katika halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga
inafanya uchunguzi juu ya Ukatili aliofanyiwa Mtoto wa miaka Miwili
Helena Joseph ambaye inadaiwa kuteswa kwa kuchomwa moto na Mama yake wa
Kambo.Kwa mujibu wa afisa ustawi wa Jamii wa halmashauri hiyo Regina
Nkwabi juhudi zinafanyika kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo
cha Dawati la Jinsia ambapo anayetuhumiwa kufanya kitendo hicho Helena
Paul anahojiwa kuhusu tukio hilo.Nkwabi amesema mtoto huyo kwa sasa
anaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama, huku hali
yake ikielezwa kuwa sio nzuri kutokana na kuwa na majeraha katika mwili
wake na vidonda kichwani.
Amesema
Taarifa za awali zinaeleza kwamba mtoto huyo ameonekana kuathiriwa
kutokana na kupigwa mara kwa mara huku akichomwa moto katika mwili wake
na kwamba wanasubiri taarifa kutoka katika hospitali ili kujua mtoto
huyo amezidiwa kiasi gani.
Inadaiwa
Mama mzazi wa mtoto huyo ambaye amefahamika kwa jina Moja la Nyamizi
alimpeleka mtoto huyo kwa baba yake mzazi ambaye anaishi na Mke mwingine
ambaye ndio mtuhumiwa ili aishi huko kutokana na kwamba yeye pamoja na
mtoto walikuwa wagonjwa.
Waandishi
wa habari waliambatana na dawati la Jinsia, ustawi wa Jamii pamoja na
shirika lisilokuwa la kiserikali la kutetea haki za Binadamu wilayani
Kahama SHIHABI, kwenda kumtafuta mama mzazi wa Mtoto huyo ambaye anaishi
Bukondamoyo ambapo hakupatikana.
Mmoja
wa Majirani wa mama huyo Matrida Lucas amesema mtoto huyo takribani
wiki tatu wakati anapelekwa kwa baba yake alikuwa mgonjwa lakini hakuwa
na majeraha kama aliyonayo kwa sasa.
Juhudi
za kumtafuta baba mzazi wa Mtoto huyo Joseph Mkazi wa Bukondamoyo
hazikuzaa matunda kutokana na kwamba amekwenda Porini kukata mkaa.
Katibu
msaidizi wa Shirika la SHIHABI Mohammed Sukwa amesema Wataendelea
kushirikiana na Usitawi wa Jamii kwa kuhakikisha kwamba sheria inachukua
mkondo wake kwa mtu atakayebainika anakosa kwani ni kinyume cha sheria
za haki za Binadamu.
0 comments:
Post a Comment