SIMULIZI: SITASAHAU NILIVYOOPOA CHANGUDOA JINI.......SEHEMU YA KWANZA

Mtunzi: Cox Dawa Yao
Simulizi: Sitasahau Nilivyoopoa Changudoa Jini........Sehemu Ya Kwanza
Nilivyomaliza masomo yangu ya kidato cha nne kuna kaka yangu alinipigia simu akaniambia kama sina kazi ya kufanya Mbeya ni bora nije jijini Dar es salaam niwe nasaidiana naye shughuli ndogo ndogo niweza kutengeneza pesa itakayonisaidia kwenye mambo yangu, nilifurahi sana kaka yangu alivyoniita Dar es salaam sababu siku zote nilikuwa natamani sana na mimi nilione jiji nilikuwaga nasikia tu watu wakisimuliana mambo ya Dar mimi nilikuwa sijawahi kufika kabisa.
Kesho yake mapema nilipanga nguo zangu kwenye begi vizuri nikaandaa kila kitu kaka yangu akanitumia pesa nikaenda kukata tiketi bila kuchelewa nikaanza kuwaaga ndugu na marafiki baadhi walisikitika sana sababu walikuwa wameshanizoea hata mimi nilisikitika sana kwenda kukaa mbali na ndugu zangu na rafiki zangu ambao nilikuwa nimezoeana nao sana. Kesho yake mapema niliwahi stendi kuu na begi langu nikaingia ndani ya basi mda ulivyofika safari ikaanza nilitamani hata gari lipae nifike haraka Dar es salaam na mimi nilione jiji ambalo kila siku nilikuwa nasikia tu mambo yake, Mungu alisaidia tulifika salama ilikuwa ni jioni nikampigia kaka yangu simu akaniambia anikute getini pale ubungo nilikaa pale kwa wasiwasi sana sababu nilishasikiaga kuwa kuna wezi na matapeli kila aliyekuwa ananiangalia nilihisi ameshajua mimi mgeni wa jiji anataka kuniibia na kilichonishangaza zaidi ni wingi wa magari na watu hayo mambo ya foleni na wingi wa watu kama ule usiku kama ule kule Mbeya vijijini nilipotokea hayakuwepo kabisa ndio maana nilikuwa nashangaa. Kaka yangu alifika pale Ubungo nikamuelekeza nilipokaa akanifuata alifurahi sana kuniona tukasalimiana pale akanisaidia kubeba begi hadi kwenye stendi ya Daladala akaniambia "Mdogo wangu huku Dar mda kama huu magari ya shida sana huwa tunagombania kwa hyo jitahidi kuwa fasta ikija gari ya Mbagala tupande tuwahi nyumbani"
Nikamjibu "sawa kaka nimekuelewa" niliitikia tu ila sikuelewa kwanini amesema wanagombaniana kupanda gari wakati nilishazoea nilipotokea Mbeya vijijini tunapanda tu kiustarabu hata iwe usiku vipi hakuna kugombania magari"
Ilikuja Daladala pale broo akaniambia ndio ya Mbagala alihakikisha mimi nimeingia ndani ya Gari na yeye ndio akapanda kulikuwa na fujo sana pale kwenye kuingia ndani ya gari na gari lilikuwa limejaa sana joto lilinitesa ndani ya gari mwili mzima uliloa jasho mimi nilishazoea baridi, tulifika Mbagala kaka yangu akachukua bajaji tukapanda hadi alipokuwa anaishi alikuwa amapanga chumba kimoja na sebule.
Aliniandalia maji nikaoga akaenda kuninunulia chakula nikala tukaanza kupiga stori nikawa namuhadithia mambo ya nyumbani alifurahi sana kaka yangu, akaniambia "mdogo wangu mimi nimekuita hapa Dar es salaam uje upige kazi utafute maisha hapa Dar kama upo siriasi na kazi lazima utafanikiwa ila ukileta tu mchezo umepotea kuna vishawishi vingi sana usije ukajiingiza kwenye mambo ya ajabu badae mimi nipewe lawama kuwa bize na kazi tu mambo mengine achana nayo"
Nilimsikiliza broo kwa makini nikamjibu "sawa kaka nimekuelewa mimi nitapiga kazi tu mambo mengine siwezi fanya kabisa nimekuja huku kwa ajili ya kutafuta maisha"
Akaniambia "basi poa mda huu tulale kesho nitakupeleka sehemu ya kazi uanze kujifunza kidogo kidogo uyazoee mazingira"
Tuliingia kulala huku nina furaha ya ajabu sikutegemea kabisa kama ipo siku na mimi nitaishi Dar es salaam pia nilifurahi kaka yangu kaniita kanipa na kazi ya kujiingizia pesa . Asubuhi broo aliniamsha akaniambia nikaoge nijiandae tuende huko kazini nikapaone, nilioga haraka nikajianda yeye alikuwa tayari kajiandaa tukaanza safari ya kwenda huko kazini kaka yangu alikuwa ana maduka mawili ya kuuza cd akaniambia anataka mimi niwe nalisimamia moja
Nilikuwaga tu nasikia Dar kuna warembo wa kila aina ile siku ya kwanza tu nilianza kuamini sababu Daladala tuliopanda na broo tulipanda na wasichana wazuri sana na hata nilivyokuwa nachungulia dirishani pia nilikuwa nawaona warembo wengi sana na masharobaro wa kila aina wakati kule kwetu nilikotokea walikuwa adimu sana

Itaendelea

0 comments:

Post a Comment