Nyota wa muziki wa Pop kutoka Canada Justin Bieber amepewa adhabu ya kuwekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miaka miwili ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za kijamii kwa kosa la kurusha mayai kwenye nyumba ya jirani yake.
Mahakama ya California pia imemwamuru mwanamuziki huyo kulipa kiasi cha dola 80,900 kwa uharibifu,kutumikia siku tano za kufanya shughuli za kijamii na kuhudhuria programu ya kudhibiti hasira.
Bieber mwenye umri wa miaka 20 hakuwepo mahakamani wakati adhabu hiyo inatolewa.
Mwimbaji huo anakabiliwa na kesi mbili za kihalifu mjini Florida na Toronto.
0 comments:
Post a Comment