AJALI YAUA MMOJA DODOMA, MWANAMKE AGONGWA NA KUFARIKI PAPO HAPO


 Watu wakiuangalia mwili wa mtu ambaye hakufahamika jina jina lake baada kugongwa na gari lisilofahamika na kufa papo hapo, katika eneo la bohari ya mkoa kati ya bunge na kituo cha mabasi yaendayo mikoani, barabara ya Morogoro - Dodoma.

 Polisi wa usalama barabarani wakisaidiana na wananchi kuupakia mwili wa mtu aliyekutwa amegogwa na kufa papo hapo na gari ambalo halikujulikana baada ya kukimbia katika barabara ya Morogoro - Dodoma karibu na jengo la bunge la Tanzania. 
Na John Banda, Dodoma

MWANAMKE asiyefahamika wa umri wa makamo amepoteza maisha baada ya kugongwa na gari aina ya Coster linalofanya shughuli za Daladala kati ya Udom Nanenane ambalo halikufahamika namba zake za usajili na kisha Gari hilo kutokomea kusikojulikana.
Kwa mujibu wa mashuhuda walioshudia tukio hilo wamesema majira ya saa 2. 30 walishuhudia kishindo kikubwa Barabarani eneo la Bohari karibu na kipitashoto kilichopo kituo cha mabasi yaendayo mikoani mjini Dodoma, ambapo baada ya kishindo hicho gari hilo liliendelea na safari zake. Mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Baraka amesema hakumuona mtu huyo wakati anavuka bali aliona Costaer hiyo mita chache kabla ya kusikia kishindo hicho na kilichomfanya ajue kuwa
ni mtu kagongwa ni kutokana na gari la nyuma kumulika mwanga ndipo alipoona tairi ya nyuma ikimalizikia kumkanyaga na kufa hapohapo.
Mkaguzi wa polisi wa usalama Barabarani Methew Mtakije  aliyefika kushuhudia tukio hilo alisema tukio hilo lilisababishwa na mwendo kasi wa Dereva wa gari hilo ambaye alikiuka sheria za usalama barabarani ambazo zinamtaka kila dereva kuendesha spidi 50 kwa saa wanapokuwa
mijini.
MtakijaAmesema mwendo kasi ni hatari  wakati wowote hasa nyakati za usikukutokana na muono mdogo unaosababishwa na giza hivyo madereva wotewazingatie sheria zilizopo ili waweze kuepusha ajili, na kuahidi kulisakagari hilo mpaka kulipata. Mwili wa Marehemu huyo ambae bado hajafahamika umehifadhiwa katika chumba cha maiti kilichopo katika hospitali yamkoa wa Dodoma.

0 comments:

Post a Comment