Chid Benz, Dudubaya, TID: Kama ngumi Piganeni na Matumla, Kaseba au Ckeka.... Mwanamke hapigwi, Msituachie Ngeu watoto wa wenzenu

Mwandishi: Joyce Kiria.
Ukatili wa kijinsia haukubaliki hata kidogo,
wengine tunapambana usiku na mchana
kutokomeza vitendo hivi vya Ukatili na
Udhalilishaji, cha ajabu watu maarufu
sasaivi wamechachamaa kuendekeza
vutendo hivyo..

Mara Dudubaya kampiga Mke wake, mara
Tid kamtukana RayC, Mara Chidbenz
kampiga mzazi mwenzake, mara Ezden
kampiga mkewe, mara Chidbenz kampiga
RayC!!!! jamani jaman jamani kwanini
mnachukua uamuzi huo wa kudhalilisha
Wanawake???
ChidBenz, Tid, Ezden na Dudubaya nyie ni
vioo kwenye jamii yetu, kwahiyo si vyema
kufanya vitendo vya kuwapiga Wanawake
na kuwadhalilisha...kwani nyie hamkoseagi?
kuna siku mmepigwa? sisi sote ni watu
wazima kwa hiyo kama tumeshindwana
kila mtu anachukua 50 zake kwa Amani.....
Kuna msemo unasema kwamba Mwanaume
wa kweli hapigi Wanawake wala
kumdhalilisha Mwanamke kwa sababu
Wanawake ni Mama zenu. vitendo
mlivyowafanyia hao Wanawake mngependa
Mama Zenu wafanyiwe???
Ushauri: Kama wewe unajiskia kupigana
basi ni vyema ukaomba pambano na
Matumla, Kaseba au Cheka ili tujue kama
kweli wewe ni mpigaji..kinyume na hapo ni
kuonea Wanawake na kuwadhalilisha
kijinsia....
Nawaheshimu sana kama wasanii lakini
naomba mjirekebishe tena kuanzia sasa
muwe mabalozi wa Kupambana na vitendo
vya Ukatili na Udhalilishaji kwa Wanawake.
na muwaombe radhi wale mliowapiga na
kuwadhalilisha..
Nipo tayari kushirikiana na nyie
kuhakikisha kuwa tunatokomeza vitendo
vya kikatili na udhalilishaji kwa
wanawake.....
Ney wa Mitego naomba useme na hawa
mastaa wenzako ambao naona hawajasikia
ule ujumbe wako kwamba Mwanamke
hapigwi na mangumi na mateke...Waeleze
Mwanamke anapigwa na nini...
Nakuita pia Linex utukumbushe ule ujumbe
wako kwamba ndoa haivunjwi na
mwanamke pekee bali hata Mwanaume nae
aweza vunja ndoa.
Sasa inapotokea mmeshindwa kuelewana
au kukubaliana haifai utumie Nguvu dhidi
ya Mwanamke wako.. Kama mkishindwana
mnaachana kwa Amani, msiachane na
kutuachia Mangeu...

0 comments:

Post a Comment