CHUMBANI ZAIDI: KWANINI WAJUZI WA MAMBO NDIO WANAOCHEMKA NA KUMWAGWA KATIKA MAPENZI

Kwenye suala la kuachika/acha/achwa
haliegemei sana kwenye kuyajua mambo
kitandani, kwani Ndoa au Mahusiano sio
Ngono pekee.
Natambua kuwa Makungwi
wengi wa "Kizazi Kipya" wanafunza
mwanamke kuonyesha mapenzi na mavituzi
ili asiachwe....na sio Maisha ya Ndoa, Uzazi
n.k.Nadhani "ukitaka usiachwe" ni "Brand"
inayouza sana, kwa sababu kila mtu hataki
kuachwa au hataki Ndoa yake "ifeli" ndani
ya miaka michache....wote wanataka Ndoa
zao zidumu muda mrefu. Lakini wanasahau
kuwa umri mkubwa wa Ndoa au Uhusiano
sio kielelezo cha furaha au mafanikio
kwenye Ndoa husika.Baadhi huendelea
kubaki kwenye Ndoa kwa sababu nyingine
na sio Mapenzi, wengine huendelea kubaki
kwenye ndoa kwa vile wanadhani umri
mfupi wa Ndoa zao ni aibu kwenye jamii
n.k.
Ili Uhusiano au Ndoa iwe yenye furaha
inahitaji Nguzo kuu 5 ambazo ni
Maelewano/Makubaliano, Mawasiliano,
Heshima, Uvumilivu na Ushirikiano....Mengine
yote hujitokeza humo.
Nguzo moja kati ya hizo ikikosekana hakika
Ndoa au Uhusiano utayumba. Sasa mmoja
asipotoa Ushirikiano kwenye Mawasiliano ili
kuwe na Maelewano, amani na furaha
hutoweka.
Hata kama unayajua sana Mambo kitandani,
huwezi kuendelea kuishi na mtu asiekupa
ushirikiano, asie kuheshimu, kukupenda n.k.
Kama umejitahidi kufanya yote au mengi
uliyofundwa kama mke lakini Mume
haonyeshi kuelewa au kutaka kubadilika ili
muendelee kufurahia Muungano wenu then
ni bora kutoka Ndoani.Hivyo nadhani hao
Makungwi ndoa zao zimefeli kwa sababu
nyingi tofauti lakini wapo ni kutokupata
ushirikiano kutoka upande wa pili.
Kwasababu mwanamke kafundwa haina
maana ndio awe mtekelezaji wa mahitaji
yote muhimu kwenye Ndoa.
Ndoa ni umoja, Ndoa ni Timu....ndoa ni kuwa
tayari kujifunza na kubadilika inapobidi ili
muendane

0 comments:

Post a Comment