Mtoto Miseto (8), anayedaiwa alikuwa
akifanya kazi za ndani kwa mama mmoja
aliyejulikana kwa jina la Mary Jerald mkazi
wa Kijiji cha Busurwa, Wilaya ya Rorya,
mkoani Mara ameokotwa ufukweni mwa
Ziwa Victoria Juni 28, mwaka huu akiwa
amejeruhiwa na anayedaiwa ni bosi wake.
Taarifa kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo,
Akeyo Thomas ambaye ni mchuuzi wa
samaki katika maeneo hayo alidai kwa
wakati akiwa na wachuuzi wenzake
walimuokota mtoto huyo akiwa amelala juu
ya mchanga ufukweni mwa ziwa hilo huku
akiwa na majeraha mbalimbali mwilini.
Akizugumza na mwandishi wetu wiki
iliyopita kwa njia ya simu na kuthibitishwa
na mmoja wa askari wa Kituo cha Polisi cha
Busurwa, alisema siku hiyo saa 12 asubuhi
walimuona mtoto akiwa amelala juu ya
mchanga huku akiwa na rundo la nguo
ambazo alidai aliambiwa na bosi wake
azifue.
"Tulimuuliza mtoto huyo sababu za kuwa
na majeraha, akajibu kuwa amejeruhiwa na
bosi wake anayeitwa Mary," alisema
Thomas.
Aliongeza kuwa, walipomchunguza
walimkuta na majeraha makubwa
kichwani, mikononi na sehemu zingine za
mwili huku akiwa amedhoofu kutokana na
njaa.
"Tuliamua kumchukuwa na kumpa chai na
maandazi, tukampeleka kituo cha polisi
akafunguliwa jalada la kesi namba NYG/
RB/52/2014 ambapo alipelekwa hospitali,
baadaye bosi wake alikamatwa," alisema
Thomas.
Polisi wa kituo hicho wamethibitisha
kukamatwa bosi wa mtoto huyo, hata
hivyo, hawakuwa tayari kueleza chochote
kwa madai kuwa wao siyo wasemaji.
0 comments:
Post a Comment