Jaja
akipokea nakala ya mkataba wake kutoka kwa Katibu Mkuu wa Young
Africans Bw Beno Njovu leo maraa baada ya kusaini kuitumikia kwa miaka
miwili
HATIMAYE mshamabuliaji Geilson
Santos Santana “Jaja” raia wa Brazil leo amesaini mkataba wa miaka
miwili (2014-2016) kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya
michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano
ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.
Katibu mkuu wa Young Africans Bw
Beno Njovu amesema usajli wa Jaja unakua ni wa pili msimu huu kwa
wachezaji wa kimataifa baada ya awali kumsajili kiungo mshambuliaji
Andrey Coutinho ambaye pia ni raia wa Brazil.
“Kazi yetu uongozi ni kutekeleza
maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa mapendekezo
ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili yote
tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi” alisema Beno.
Jaja ambaye alizaliwa tarehe 21
Septemba 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju nchini Brazili mpaka
anasajiliwa na timu ya Young Africans alikuwa akiichezea timu ya
Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo mwenye mwili
uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu katikati ya wiki
iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake Leonado
Neiva ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha Young Africans kwa ajili ya
michuano mbalimbali.
Chanzo: Tovuti ya Yanga
0 comments:
Post a Comment