Mume
wa mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Frola Mbasha,Mr.Emanuel Mbasha
leo amepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala
kujibu mashtaka mawili yanayo mkabili ya ubakaji.Katika kesi hiyo
inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika kuhairisha kesi hiyo
kwa muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha kwamba ana wakili wa
kumtetea lakini alishindwa kufika kutokana na matatizo ya usafiri.
Kauli
hiyo ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa na nia
ya kuwa na wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani ilionekana tangu
kesi hiyo ianze Mbasha hakuwai kusimamiwa na wakili.
Mara
baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake
kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani
Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.Emanuel Mbasha ana kabiliwa na
kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda makosa hayo maeneo ya
Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha alisindikizwa mahakamani na
ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha kutoonekana Mahakamani na badala yake
alionekana mdogo wake Flora ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment