IKIWA
takribani mwezi mmoja baada ya Mahabusu wanane wa gereza la wilaya ya
Geita mkoani Geita kuvua nguo na kubaki utupu katika mahakama ya Mwanzo
ya Nyankumbu kwa madai ya kucheleweshwa kesi zao huku wakitaka mamlaka
husika ikiwa mwanasheria wa serikali ,jaji na mkuu wa mkoa wawasikilize
madai yao hatimaye kesi zao zimeanza kusikilizwa jana katika mahakama ya
wilaya.Mbele ya Hakimu wa
mahakama ya wilaya Kario Mrisho ,wakili wa serikali Erasto Anosisye
alidai kuwa kati ya mahabusu wanana,wanne wana kesi ya mada na wanne
wana kesi ya kuvunja na kuiba ambayo imeanza kusikilizwa huku wa kesi ya
mada inasubiri mahakama kuu kwa vile mahakama ya wilaya haina uwezo wa
kusikiliza kesi hizo.
Katika
mashitaka ya kuvunja na kuiba inadaiwa kuwa washitakiwa ambao ni
Iriza Warioba(26) mkazi wa katundu,Joseph Mrefu(28) mkazi wa
Runzewe,Silvester Emmanuel(22) mkazi wa katundu na Saimon Panya(22)
mkazi wa msufini mjini Geita mnamo tarehe 3 mwezi 11 2013 majira ya saa
tatu usiku katika kijiji cha Nyamulilima kata ya Mtakuja wilayani Geita
watuhumiwa walivunja na kuiba solar power 2,Betry 5,tv,na vifaa vingine
kwenye kampuni la ujenzi ya Hircon Construction Compay inayofanya kazi
katika mgodi wa Geita Gold Mine vyenye thamani ya shilingi
19,530,000/=na kutokomea kusikojulikana.
Aidha
mara baada ya kukimbia kusikojulikana mlinzi aliyekuwepo siku hiyo
alienda kutoa taarifa na baada ya mda mfupi walifuatiliwa na kukamatwa
na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Mgusu kabla hawajapelekwa
mahakamani.
Baada
ya kusomewa mashitka yao watuhumiwa wote wanne walikana kosa hilo na
hakimu Mrisho aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 31 mwezi huu huku
watuhumiwa wakirudishwa rumande baada ya kukoswa vigezo vya dhamana.
Watuhumiwa
hao mwezi uliopita walileta tafrani baada ya kunga'anga'nia mlingoti wa
bendera huku wakiwa uchi walipokuwa wameletwa mahakamani kusikilizwa
kesi zao wakidai kuwa wamekuwa wanakuja mahakamani bila ya kusikilizwa
kesi zao hivyo hawajui hatma yao na kumtaka mkuu wa mkoa na viongozi
wengine wanaohusika wawasikilize.
Hata
hivyo katibu tawala wa wilaya alifanikiwa kuwaelewesha na kutoka hapo
kwa ahadi ya kutatua kero zao ambapo siku hiyo jopo la mahakimu wa
wilaya na mahakama ya mwanzo,mwanasheria wa serikali pamoja na ofisi ya
upelelezi mkoa walienda katika gereza hilo mnamo saa 8 na kusikiliza
kero zao wote na ambao hawakugoma wakiwemo wafungwa na mahabusu.
0 comments:
Post a Comment