Meneja
wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akimkabidhi vifaa Makamu
wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange. (Picha: Executive Solutions).
Meneja
wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akimkabidhi vifaa
Mkurugenzi wa Masoko wa Yanga, George Simba. Anayeshuhudia ni Hafidh
Saleh, Meneja wa Yanga. (Picha: Executive Solutions).
Meneja
wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiwakabidhi vifaa Makamu
wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa
Yanga George Simba (Picha: Executive Solutions).
Ikiwa ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager
imekabidhi vifaa vya michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young
Africans SC kwa ajili ya msimu wa 2014/15 wa Ligi Kuu inayotarajiwa
kuanza mwezi ujao. Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George
Kavishe alisema “Tunawapatia vifaa mapema kabla ya ligi kuanza ili
wapate muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2014/15 ambayo
bila shaka itakuwa na changamoto kubwa kwa timu hizi mbili na pia
tunaamini kuwa siri ya mafanikio katika michezo ni maandalizi mazuri. Ni
matumaini yetu kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa Simba na Yanga
wataiwakilisha Kili vizuri na kufurahia kuzichezea klabu hizi kongwe.”
Kavishe aliongeza kuwa Vifaa ambavyo leo tunatoa ni pamoja na mipira,
viatu, soksi, shin guards, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na
vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu hizi za Simba na Yanga
kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya juu. Kilimanjaro
Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji
kinachoongoza katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba
uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza
mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea kutimiza wajibu wetu kwa klabu
hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha tunalifikisha soka la
Tanzania kwenye kilele cha mafanikio. Kavishe alisema kuwa udhamini wa
Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na Yanga umelenga kukuza soka la
Tanzania, kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na
vilevile kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya
kimataifa. Tunawashukuru viongozi wa Simba na Yanga, mashabiki wote,
vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri
tunaoendelea kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio
ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili maarufu. “Tunawaomba mashabiki wa
Simba na Yanga waendelee kuiunga mkono bia yao ya Kilimanjaro Premium
Lager kwani tunafanya kila jitihada kuwapa burudani na kufikisha soka la
Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.”
0 comments:
Post a Comment