Kinara wa Madawa ya Kulevya Zanzibar Akamatwa Uwanja wa Ndege na gramu 5000 za Unga

Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Ali Suleiman Rashid(34) akiwa
na mikoba 14 ya wanawake aliyohifadhia dawa za kulevya zenye uzito wa
kilo tano akitokea Oman katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid
Amani Karume visiwani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika
Makao Mkuu ya Polisi Ziwani mjini Zanzibar, Naibu Mkurugenzi wa
Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI ), Yussuf Ilembo alisema kuwa
mtuhumiwa huyo raia wa Tanzania amekamatwa muda mfupi baada ya
kushuka kutoka Ndege ya Oman yenye namba za usajili .WY.717 iliyokuwa
ikitokea Muscat.Ilembo alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Julai 9, saa
8 mchana akiwa amehifadhi mikoba hiyo katika sanduku kubwa lenye rangi
nyeusi na maofisa wa upelelezi waligundua ndani yake kuwemomikoba 14
iliyokuwa na dawa hizo ikiwa imeshonewa kwa vitumaalumu."Dawa hizo za
kulevya zina uzito wa kilo 5.605, zilihifadhiwakwenye mikoba 14
inayotumiwana wanawake. Upelelezi kukamilika, atafikishwa mahakamani
mara moja," alisema DCI Ilembo.Alisema polisi inaendelea na uchunguzi
wake ili kusaka mtandao wa watu wanaojishughulisha na vitendo hivyo
kwa kuchunguza njia mbalimbali za mawasiliano za mtuhumiwa huyo
aliyekamatwa.Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia
hati ya kusafiria namba AB 363906 iliotolewa Desemba 29 mwaka 2009
Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Dar es Salaam na tayari ameshasafiri
katika nchi za Brazil, China, Japan, Hong Kong, Afrika Kusini na Falme
za Kiarabu.Ilembo aliwataka wananchi kuchukua hatua kwa kushirikiana
na Jeshi la Polisi ili kuwafichua kwa siri, wanaoingiza dawa za
kulevya na wauzaji ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.'Wakati wa
kulindana, kuleana na kuoneana aibu umekwisha, kila mmoja ajione ana
wajibu wa kulilinda taifa kwa maisha yake na vizazi vijavyo,"alisema
DCI Ilembo.Mapema mwaka huu polisi walikamata mabegi mawili yakiwa na
dawa za kuelvya katika chumba cha kuondokea abiria, Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

0 comments:

Post a Comment