KLABU ya Yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba za Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya wachezaji wake kupitia program maalumu.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa NSSF, Crecentius Magori alisema wachezaji wanapaswa kuona fahari kumiliki nyuma au ardhi mjini, si magari.
Magori alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wachezaji wa Yanga ambao walikuwepo katika utiaji wa saini makubaliano hayo, kuchangamkia mradi huo uliopo makao mapya katika Kijiji cha Dege, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
“Sisi tuko tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo za kisasa zaidi, hivyo ningependa kuwashauri mpatapo fedha za mikataba, mkitoa kiasi nanyi muwe wamiliki wa nyumba hizo. “Kama utamudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8 na kulipa kwa miezi mitatu mfululizo, NSSF watawapa ufunguo na kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi kwa miaka 15, kisha unakuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo,” alisema Magori. Aliongeza kuwa hata ikitokea mchezaji akafariki dunia, nyumba hiyo itaendelea kuwa mali ya familia ya mhusika kwani itakuwa imerithiwa huku akisihi wachezaji ambao si wanachama wa NSSF, kujiunga ili kupata manufaa ya shirika hilo. Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alisema makubaliano hayo ni matokeo ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau. Alisema lengo ni kuhakikisha kila mchezaji wa timu hiyo anawezeshwa kumiliki nyumba ikiwa ni moja ya mali ya kudumu ambayo itakuwa na manufaa yake wakati anacheza, hata baada ya kustaafu soka
KATIBU MKUU WA YANGA, BENO NJOVU, ALIKUWEPO.
MAXIMO, MSAIDIZI WAKE LEIVA, SALVATORY EDWARD WAKISIKILIZA KWA UMAKINI MKUBWA.
MPOGOLO NA JACOB, WALIKUWEPO.
BAADHI YA MIJENGO.
0 comments:
Post a Comment