MCHEZAJI
mpya wa Liverpool, Emre Can alicheza kwa dakika 21 tu timu hiyo
ikipata ushindi wa kwanza bila mshambuliaji Luis Suarez aliyehamia
Barcelona.
Can,
aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 10 kutoka Bayer Leverkusen msimu huu
alianguka chini na kuanza kushika misuli ya mguu wake kulia.
Lilikuwa ni pigo kubwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anayeandaliwa kuwa mrithi wa Steve Gerrard. Preston ya Daraja la Kwanza, ilipata bao la kuongoza kupitia kwa Josh Brownhill mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Licha
ya mchezo huo kuonyeshwa na BT Sport, ulikuwa na idadi kubwa ya
wachezaji waliobadilishwa, 47 (23 kwa Liverpool na 24 kwa Preston).
Suso,
aliisawazishia Liverpool katikati ya kipindi cha pili kabla ya Kristoph
Peterson kufunga la ushindi dakika 14 kuelekea mwisho wa mchezo.
0 comments:
Post a Comment