MAMBO MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUTENDWA NA UMPENDAE

KATIKA MAISHA YA KIMAPENZI HAKUNA KITU KINACHOUMA KAMA KUSALITIWA, TENA KUSALITIWA KUNAKOUMA ZAIDI NI PALE UNAPOBAINI MPENZI WAKO KAMPA PENZI MTU UNAYEMJUA HALAFU UKIJILINGANISHA WEWE NA HUYO ALIYEPEWA UNASHINDWA KUELEWA KILICHOMSHAWISHI MPENZI WAKO KUMPA PENZI HUYO MTU...
Lakini licha ya kwamba usaliti si kitu kizuri, watu wamekuwa wakisalitiana, tena sana tu. Inafika wakati unashindwa kuamini kama yupo mtu ambaye hajawahi kumsaliti mpenzi wake....Niseme tu kwamba wapo wachache waliotulia ila asilimia kubwa ya walio kwenye uhusiano ni wasaliti hata tafiti zimethibitisha hilo. Kama hali yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza ni kwamba unapobaini mpenzi wako kakusaliti ni kipi unachotakiwa kufanya? Je, ni kuamua kunywa sumu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wengine? Sidhani kama huo ni uamuzi sahihi. 

0 comments:

Post a Comment