Harnaam Kaur, mwanamke mwenye umri wa miaka 23 anayeishi katika mji wa
Slough, Kusini Mashariki mwa Uingereza amepokea vitisho vya kuuawa
kutoka kwa watu asiowafahamu kwenye mitandao kwa sababu ya ndevu zake
nyingi zinazomfanya asitofautishwe kirahisi na mwanaume.
Mwanamke huyo ambaye anakabiriwa na tatizo la kuwa na vinyweleo vingi
kupita kiasi, tatizo linalojulikana kitaalamu kama ‘polycystic ovary
syndrome’, ameeleza kuwa alianza kupata tatizo hilo akiwa na umri wa
miaka 11 na kwamba alikuwa akizinyoa mara mbili kwa wiki.
Ameeleza kuwa alipokuwa shuleni alikuwa akionewa sana kwa kuitwa majina
mengi ya kejeli kama ‘jike dume’, na kwamba alikuwa anashindwa hata
kuwaangalia watu usoni na alipotoka shule alijifungia ndani siku zote
asionekane mara kwa mara.
Ameongeza kuwa kutokana na kuishi katika hali hiyo alifikia hatua akafikiria kujiua.
Hata hivyo, Harnaam amesema kuwa amejiunga na dini ya Sikh na
kubatizwa, na kwamba imani ya dini hiyo hairuhusu watu kunyoa vinyweleo
vyao kwa kuwa Mungu ndiye aliyewaumba hivyo. Kwa hiyo ameziachia nywele
zake na sasa anaonekana kama mwanaume akiwa na nywele nyingi kidevuni,
mikononi na kifuani.
Imani hiyo imempa ujasiri zaidi juu ya muonekano wake, na anajiona mwanamke mwenye mvuto zaidi.
“Nahisi nimekuwa mwanamke zaidi, nina mvuto zaidi na nadhani naonekana
hivyo pia. Nimejifunza kupenda jinsi nilivyo na hakuna kitakachonitikisa
sasa hivi.” Amesema Harnaam.
“nawezza kwenda kwenye maduka ya wanawake bila kuhisi kuwa sitakiwi
kuwa kule. Navaa skirts, gauni na vidani na napenda kutengeneza kucha
zangu kama msichana mwingine yeyote
0 comments:
Post a Comment