Mganga wa Jadi anaswa Gesti na Wake za Watu......Alikuwa akiwatengenezea dawa kwa kuwavua Nguo Zote Kisha kuwachezea Nyeti zao
Mganga wa jadi almaarufu sangoma
aliyetajwa kwa jina la Wadebi Jinasa
amepata aibu ya karne baada ya kunaswa
'live' na wake za watu kwenye gesti moja
(jina linahifadhiwa) iliyopo Tandika jijini Dar
es Salaam.
Tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo hayo,
usiku wa manane wa kuamkia Jumanne
iliyopita, wakati waumini wa Dini ya
Kiislamu waliofunga kwa ajili ya Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani wakila daku.
Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo
alidaiwa kuwa alikuwa akiwafanyia wake
hao wa watu dawa ya mapenzi kwa
kuwavua nguo zote kisha 'kuwachezea'.
Ilidaiwa kuwa mbali na kuwachezea,
amekuwa akiwafanyia mchezo usiofaa
mmoja baada ya mwingine.
Chanzo cha sakata hilo kilidai kuwa
sangoma huyo amekuwa na tabia hiyo hasa
akimuona mwanamke mwenye mvuto
katika hali ambayo haikueleweka mara
moja humuita majina yake matatu, yaani la
kwake, baba hadi la babu yake, jambo
linalosababisha anayeitwa kushtuka na
kuhisi mtu huyo atakuwa anamfahamu
kiundani.
Ilidaiwa kuwa baada ya mwanamke huyo
kusimama huanza kumwelezea matatizo
yake na kumtajiwa hadi matatizo
yanayowapata ndugu zake walio vijijini na
sehemu nyingine za mbali.
Kiliendelea kudai kwamba, sangoma huyo
amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa
kuwatajia matatizo yao sawia bila kukosea
hivyo kuwachanganya na kumjengea imani
kuwa ni 'fundi' wa masuala hayo.
Kufuatia vituko vyake, juzikati mume wa
mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa),
Huruka Hassan alirejea nyumbani kwake na
kukuta mkewe hayupo.Alidai alipofanya
uchunguzi wa haraka, aligundua ameenda
kwenye gesti hiyo kupata tiba.
Sangoma akiwa na mawazo baada ya
kunaswa.
Ilidaiwa kwamba, siku zote Huruka
amekuwa akimuacha mkewe akapate tiba
lakini siku ya tukio machale yalimcheza,
alipofika kwenye gesti hiyo alijibanza
ukumbini na kusikia sauti ya mkewe
ikinong'ona chumbani na sauti ya 'besi' la
sangoma huyo kwa mbaaali.
Ilisemekana kwamba uzalendo ulimshinda
Huruka na kujikuta akivunja masharti ya
kilinge cha sangoma huyo kwa kuchungulia
kwenye tundu la kupitisha funguo.
"Haaamadi!" alisikika Huruka alimuona laivu
mkewe akiwa mtupu akitaka kufanyiwa
vitendo vichafu ambapo sangoma huyo
alidaiwa kuwa alikuwa akjiandaa
kumfanyia 'amshaamsha'.
Ilidaiwa kuwa Huruka alishindwa kujizuia,
akagonga mlango kwa hasira ambapo
sangoma alivaa 'chapchap' na
kufungua.Ilielezwa kwamba walipokutana
uso kwa uso, Huruka alitunishiana misuli na
sangoma huyo wakataka kuzichapa lakini
jamaa akaona amchukue mkewe na
kutimka naye.
Baada ya mke wa Huruka kuokolewa
kufanyiwa ukenge, mwanaume mwingine
wa eneo hilo, Tabu Abdallah naye alidai
kumnasa mkewe kwenye gesti hiyo akiwa
amekalishwa kama alivyozaliwa, akitolewa
vitu fulani tumboni na sangoma huyo.
Akizungumza na mwanahabari wetu
aliyekuwepo eneo la tukio usiku huo, Tabu
alisema alimnasa mkewe na sangoma huyo
baada ya kutonywa juu ya mkewe kuingia
gesti hiyo.
Alisema sangoma huyo alimchukua mkewe
kwa gia ya kumtibia kumbe alikuwa na lake
jambo.
Baada ya kutokea kwa mtiti huo, Mjumbe
wa Shina namba 29, Azimio-Tandika, Faraj
Neto, wanawake waliodhalilishwa, waume
zao, polisi na mmliki wa gesti hiyo,
Ebenezer Ngowo, walimchomoa sangoma
huyo kwenye gesti hiyo.
Katika hali ya kushangaza mke wa Tabu
alikuwa akimlaumu mumewe kwa kutaka
kumpiga mganga wake ambaye alikuwa
akitaka kummalizia matatizo huku
wanawake wengine wakiwaomba radhi
waume zao na kudai walirubuniwa.
Akizungumizia mkasa huo mke wa Tabu
alisema kuna siku alikutana na mganga
huyo njiani ambapo alimwita majina yake
matatu, aliposimama kumsikiliza ndiyo
akaanza kumtajia matatizo yake, jina la
mama yake mzazi na kumwambia mama
huyo huko aliko ana tatizo sugu la miguu
jambo ambalo ni kweli ndipo alianza
kumuamini.
MWISHO WA SAKATA
Mwisho wa sakata hilo, mjumbe wa
nyumba kumi alimtaka sangoma huyo
kuondoka eneo hilo na mmiliki wa gesti
hiyo alimtaka mganga huyo kuhama
kwenye gesti yake kutokana na tabia yake
ya kubadilisha wanawake.
Kwa upande wao, polisi walimshikilia
sangoma huyo kutokana na sababu za
kiusalama kufuatia wenye wake na
wananchi wenye hasira kutaka kumpiga
mawe na kumuua.
Chanzo: Gazeti la Amani/ GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment