MICHEZO; SIMBA SC YAFANYA KUFURU, YASAINI WATATU KWA MPIGO


SIMBA SC imesajili wachezaji wawili chupukizi kwa ajili ya timu yake ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Simba B, akiwemo Peter Manyika, mtoto wa kipa wa zamani wa Yanga SC, Manyika Opeter. 
Makamu Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesimamia zoezi hilo lililokamilika vyema akishirikiana na Mjumbe wa Kamati ya Usajili, Said Tuliy leo mjini Dar es Salaam.
Said Tuliy kulia, Kaburu kushoto na Manyika Jr. katikati akisaini Simba SC

Pamoja na kipa huyo wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Wekundu hao wa Msimbazi pia wamemsajili kinda mwingine kutoka Mwadui ya Shinyanga, kiungo mshambuliaji Ibrahim Hajibu Migomba, ambaye alipelekwa kwa mkopo huko msimu uliopita kutoka Simba B.
Kaburu maarufu kama Perez, amesema mtoto wa Manyika amesaini miaka mitatu sawa na Hajibu ambao wote pamoja na kusajiliwa kama wachezaji wa Simba B, watakuwa wanakomazwa kikosi cha kwanza.

Awali ya hapo, leo Simba SC ilimsajili kipa wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ aliyesaini Mkataba wa miaka miwili.
Kaburu kushoto akiwa na Hajibu baada ya kusaini

Kipa huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara amekuwa akiibeba Mtibwa Sugar kwa misimu mitatu iliyopita, tangu kuondoka kwa Shaaban Hassan Kado.
Cassillas akisaini pembeni ya Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Said Tuliy
Kipa huyo ambaye mara kadhaa huitwa timu ya taifra, Taifa Stars amesaini leo Dar es Salaam mbele ya viongozi wa Simba SC.
Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Said Tuliy kushoto akiwa na Cassilas baada ya kusaini leo

Cassilas anayeishi Mji Mwema, Kigamboni mjini Dar es Salaam anakwenda kufanya idadi ya makipa watatu Simba SC, ambao ni Ivo Mapunda na Abuu Hashim baada ya kutemwa kwa Mghana, Yaw Berko. 
Maana yake, Cassilas sasa atalazimika kwenda kuchuana na kipa mkongwe Ivo, kugombea namba katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.

0 comments:

Post a Comment