Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe
MH! Kigauni kifupi alichotinga staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline
Wolper Massawe katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kimeibua
minong’ono watu kuhoji kulikoni akivae hivyo ndani ya Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani. Tukio hilo lilowastaajabisha wengi lilijiri wikiendi
iliyopita katika Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki, Dar ambapo
asilimia kubwa ya waalikwa katika hafla hiyo walisema hakikustaili hasa
kwenye mwezi huu wa
toba. “Unajua siku zote tunaambiwa sisi Bongo Movie hatuna heshima, siyo
kweli, kuna watu wapo kwa ajili ya kutudhalilisha. Angalia Wolper
alichovaa,” alisema mwigizaji mmoja ambaye hakutaka jina liandikwe
gazetini. Alipoulizwa Wolper kuhusiana na madai hayo ya udhalilishaji,
alijibu: “Achana nao hao ni wanafiki tu kwani kuna mtu amekatazwa kuvaa
kama hivi?”
0 comments:
Post a Comment