Mtoto wa miaka 8 aiba benki kwa kutumia iPad!

Kuna baadhi ya matukio ya kivamizi tumezoea kuyaona kwenye filamu za kipelelezi huku yakituacha midomo wazi na sifa zote zinaenda kwa mtayarishaji, muongozaji na waigizaji wa filamu hiyo. Lakini hili ni tukio halisi na sio filamu, unapodhani kuna usalama wezi hubuni mbinu ambazo hata hazifiriki kirahisi.

Maafisa wa Plainfield, New Jersey, Marekani walijikuta katika wakati mgumu wakimsaka mtoto mwenye umri wa miaka 8 ambaye anadaiwa kuiba bank kwa kutumia iPad yake tu.
Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa sita mchana Jumatano June, 25 mwaka huu katika beki inayoitwa Greater Plainfield Bank & Trut. Maafisa walifika katika eneo la tukio haraka kuungana na walinzi kumsaka mtoto huyo baada ya kupigiwa simu na mkuu wa ulinzi wa bank hiyo ambapo awali walidhani alikuwa anatania.
Walipofika eneo la tukio, wafanyakazi wa benki hiyo walieleza jinsi ambavyo tukio hilo limetokea, ambapo mtoto huyo kwa utulivu alitembea hadi kwa mmoja kati ya tellers ambaye jina lake halikutajwa.
Alipofika kwa teller huyo kwa utaratibu tu alimpa iPad iliyokuwa na message juu iliyosomeka ‘giv me all of th money I hav a gun n my bookbag’. Kwa uoga mfanyakazi huyo ambaye aliishia kuuona mkono na iPad zaidi, alimkabidhi pesa zinazokadiriwa kuwa $12,000 na mtoto huyo alifanikiwa kuvuka mlango tu na kuchukua ‘motorized scoote’ akatoweka haraka kwenye jengo hilo.
Camera za jengo hilo zinamuonesha mtoto huyo aliyekuwa amevaa fulana nyekundu iliyoandikwa mbele ‘TURN DOWN 4 WHAT?’. Na anaonekana akitereza na begi lenye pesa begani kwake.
Hakuna shuhuda mwingine aliyeshtukia wakati wa tukio hilo zaidi ya mfanyakazi wa benki.

0 comments:

Post a Comment