Wanawake wenye makalio makubwa namapaja makubwa kama vile Beyonce
naJeniffer Lopez wana uwezekano mdogosana wa kupata magonjwa ya moyo
na kisukari kulinganisha na wanawake wenye makalio madogo, matokeo ya
utafiti wa wanasayansi nchini Uingereza umeonyesha. Wanasayansi wa
nchini Uingereza waliofanya utafiti wao katika chuo kikuu cha Oxford
University
wamegundua kuwa makalio makubwa yana faida kubwa zaidi
kiafya kuliko matumbo makubwa (vitambi).Utafiti umeonyesha kuwa
makalio na mapaja makubwa huhifadhi mafuta ambayo husaidia mwili
kujilinda na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo. "Mafuta ya
kwenye makalio na mapaja ni bora kwa afya lakini mafuta mengi ya
kwenye tumbo si mazuri kiafya", alisema Dr Konstantinos Manolopoulos,
mmoja wa watafiti watatu walioshiriki kwenye utafiti huo ambao matokeo
yake yalichapishwa kwenye jarida la International Journal
ofObesity.Watafiti hao walisema kwamba mafuta ya kwenye tumbo hutoa
tindikali nyingi za mafuta zenye madhara kwa mwili wakati mafuta ya
kwenye makalio na mapaja huzuia tindikali za mafuta zenyemadhara
kuingia kwenye misuli na maini na hivyo kuuepusha mwili na magonjwa ya
kisukari na magonjwa ya moyo...Ingawa mafuta ya kwenye makalio na
mapaja huyeyuka taratibu sana lakini mafuta hayo hutoa homoni zenye
faida zijulikanazo kama adiponectin ambazo huilinda mishipa ya damu na
kusimamia kiwango cha sukari mwilini.Wanasayansi hao walisema kuwa
wanaendelea na utafiti ili kutengeneza dawa za kuufanya mwili uhifadhi
mafuta yake kwenye makalio na mapaja ili kupunguza matatizo ya kiafya
yanayosababishwa mafuta kujazana kwenye tumbo. Utafiti huo ulimalizia
kwa kusema kuwa wanawake wenye mapaja au makalio madogo sana wana
uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo kadhaa ya kiafya kama vile
kisukari na magonjwa ya moyo...
0 comments:
Post a Comment