REAL MADRID YAKARIBIA KUFANYA BALAA LINGINE USAJILI, MFUNGAJI BORA KOMBE LA DUNIA MBIONI KUTUA BERNABEU

KLABU ya Real Madrid wanakaribia kufanikisha usajili wa mshindi wa kiatu cha dhahabu cha Kombe la Dunia, James Rodriguez hii ni kwa mujibu wa gazeti la Hispania la AS.
Gazeti hilo la jijini Madrid limedai kuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa tayari wameshafikia makubaliano yam domo na mchezaji wanachotakiwa kufanya sasa ni kumalizana na Monaco, ambao wanataka dau la pauni milioni 63 kwa ajili ya Mcolombia huyo.
Majadiliano hayajawa ya moja kwa moja bado, lakini Real Madrid wanatumaini kumuuza winga, Angel Di Maria kwenda Paris Saint-Germain wiki hii kwa dau la pauni milioni 47 na kuharakisha uhamisho wa James.

Anakwenda Hispania? Rodriguez anatajwa kukubaliana naReal Madrid
View from Spain: AS claim James Rodriguez is close to a move to Madrid
Safe hands: Keylor Navas is also close to joining Madrid
Matumizi: AS linadai Real Madrid wanakaribia kumnasa James Rodriguez, wakati Marca pia linadai kipa Keylor Navas anakaribia kutua Bernabeu

Gazeti hilo pia linadai kuwa Toni Kroos amefuzu vipimo pame Real na atatambulishwa Madrid muda wowote na atakuwa akivaa jezi nambaa nane.
Gazeti la jijini Barcalona, Mundo Deportivo limedai kuwa bosi mpya wa Barca, Luis Enrique anataka kujenga timu ya kutisha Camp Nou ambayo itakuwa inahamasisha na kucheza soka la asili ya klabu.
Mbele limebebwa na kicha, Enrique amesema: Messi, Neymar na Suarez?nimefurahi.
Mundo Deportivo
L'Equipe
Magazeti: Gazeti la jijini Barcelona, Mundo Deportivo linamtazama Luis Enrique na L'Equipe linasubiri usajili
Marca linadai kuwa kipa wa Costa Rica, Keylor Navas ameipotezea Bayern Munich baada ya kusikia kuwa Real Madrid inamataka.
Nchini Italia stori moja ilitawala kwenye magazeti yote matatu makubwa: Massimiliano Allegri ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Juventus.
La Gazzetta dello Sport likuwa na kichawa: The three challenges for Allegri (Changamoto tatu kwa Allegri). Wafike robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, aelewane naAndrea Pirlo na awazibe midomo wanaombeza.
Keylor Navas akifanya mazoezi balaa ya sarakasi
Gazzetta
Tuttosport
Kazi Italia: Uteuzi wa Massimiliano Allegri kama kocha wa Juventus umetawala vyombo vya habari vya Italia.
orriere dello Sport lilikuwa na kichwa: Allegri – Mashabiki wagoma, miaka miwili na kiapo cha kuwashawishi mashabiki… kufika mbali Ligi ya Mabingwa.
Tutosport ilikuwa na kichwa hiki: Kila la kheri Allegri: ‘Nitafanikiwa kuwashawishi mashabiki kwa kujituma, uweledi na matokeo – niko hapa kushinda.”
Pia walidai kuwa AC Milan wanaisaka saini ya Nani kutoka Manchester United na Domenico Criscito kutoka Zenit St Petersburg.
Pande za Ufaransa, mashindano ya baiskeli ya Tour de France ndiyo yalitawala kurasa ya mbele ya gazeti la L’Equipe, lakini pia waliandika kuhusu uhamisho wa wachezaji huku, kuhusu Sami Khedira kuhusishwa na Arsenal na Keylor Navas  na Real Madrid.

0 comments:

Post a Comment