SIMULIZI: JOHNSO NA MARIA.......SEHEMU YA NNE

Ilipoishia
Wazazi wa Maria walizidi kumtukana sana Johnson ndani ya gari Baba yake Maria akamuambia Johnson "Yani kijana tukimkuta binti yetu huku kwako leo ndo utakuwa mwisho wa maisha yako hatuwezi kukubali kijana masikini kama wewe huna mbele wala nyuma uwe mpenzi wa binti yetu''


Endelea
Yale maneno yalimuumiza sana Johnson hadi akawa anajuta kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Maria, binti ambaye kwao wana uwezo sana wa kifedha.
Johnson alitetemeka huku akimuomba Mungu amsaidie wakifika kwake wasimkute Maria sababu alihisi Maria atakuwa ameogopa kuingia kwao karudi tena nyumbani kwake
Johnson aliwafikisha wazazi wa Maria mpaka anapoishi Mama yake Maria akamuambia Johson kwa dharau "we mpumbavu hapa ndo unapoishi yani kwenye hichi kinyumba kibovu kichafu ndio unamletaga binti yetu na yeye karidhika na wewe au umemuwekea madawa binti yetu akupende"
Yale maneno yalizidi kumuumiza Johnson akajikuta machozi yanamtoka kwa zile dharau walizokuwa wanamletea wazazi wa Maria alitoa funguo akafungua mlango "Wazazi wa Maria wakaingia wakakagua sehemu zote lakini hawakumuona binti yao ila walivikuta baadhi ya vitu vya Maria alivyokuwa anaviacha kwa Johnson.
Mama yake Maria akamuambia Johnson "wewe lazima unajua binti yetu alipo leo hatukuachii binti yetu hajawahi kulala nje hatuwezi kukubali binti yetu aharibiwe na kimtu kama wewe hadi kafikia hatua ya kuacha vitu vyake huku kwako"
Johnson akawaambia "mimi binti yenu mda mrefu sana nilishaachana naye na hivyo vitu mnavyoviona aliviacha muda mrefu hadi leo hajaja kuvichukua"
Wazazi wake Maria wakamuambia "yani usitudanganye sisi sio watoto wadogo tunakupeleka polisi ukasote ndio utaongea ukweli sisi sio watu wa mchezo wewe kijana"
Wakamuambia Johnson afunge mlango wa chumba chake waelekee kituo cha polisi Baba yake Maria akamuonyesha Johnson bastola akamuambia "unaona hii kitu ukiendelea kubisha kuwa hujui binti yangu alipo nitakumaliza" Katika maisha yake Johnson hakuwahi kuona bastola ndio ilikuwa mara yake ya kwanza ilibaki kidogo mkojo umtoke akili yake ikaanza kumuambia bora aongee ukweli labda atasamehewa lakini pia akawa anawaza akiongea ukweli kuwa alilala na Maria pale kwake wazazi wa Maria wanaweza wakamfunga alijikuta amechanganyikiwa haelewi afanye nini

Itaendelea...............

0 comments:

Post a Comment