SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA.............SEHEMU YA PILI

Ilipoishia
Maria alikaa nyumbani kwa kina Johnson hadi saa 4 usiku lakini Johnson hakutokea Maria alilia sana sababu haikuwa kawaida ya Johnson kwenda sehemu bila kumuambia wala simu yake kutopatikana mda mrefu vile

Endelea
Maria alilia sana mwisho akakata tamaa akasimama alipokuwa amekaa akaanza kujiandaa kurudi nyumbani kwao na hakuwahi hata siku moja kurudi nyumbani kwao usiku kama ule. Alianza kuondoka kwa unyonge huku machozi yanamtoka kichwani kwake akijiuliza Johnson atakuwa kaelekea wapi lakini mbele yake alimuona mtu kama Johnson akiwa anakuja amebeba mzigo kichwani japo ilikuwa giza, alimtambua sababu aliujua vizuri sana mwendo wa mpenzi wake Johnson. Maria alimkimbilia kwa furaha Johnson akamkumbatia akampiga mabusu akampokea ule mzigo aliokuwa ameubeba Johnson yeye alishangaa sana kumuona Maria hajaenda nyumbani kwao hadi usiku wote ule akajua anaweza akamletea matatizo na ukiangalia wazazi wa Maria walikuwa hawampendi sana Johnson na mara kwa mara walimpa sana vitisho Johnson: we Maria mbona hadi muda huu upo huku wazazi wako si watakuwa wanakutafuta umewapa wasiwasi?

Maria: Yani Johnson mpenzi wangu mimi nilichanganyikiwa nikawa sijielewi nimetoka chuo nimekufuata gengeni kwako sikukuta, nikaja hapa kwako sikukuta pia, nimepiga simu yako hupatikana nimechanganyikiwa sana mpenzi wangu ulikuwa wapi? Johnson: mpenzi yani leo sokoni vitu vilikuwa vya shida sana nilifwata mzigo wa gengeni ndio maana umeona nimechelewa hapa nimechoka sana.
Maria: Pole sana mpenzi wangu mimi nilihisi labda umepatwa na matatizo mpenzi wangu. Johnson: kwa hiyo nyumbani kwenu unaenda saa ngapi si unajua wazazi wako walivyo wakali?

 Maria: hata usiwe na wasiwasi mpenzi mimi wazazi wangu najua jinsi gani nitawapanga mimi leo sirudi nyumbani nalala huku huku kwako. Johnson alikataa kabisa hilo swala la Maria kutaka kulala kwake walibishana sana hadi baadae ikabidi tu Johnson akubaliane na Maria Maria aliwasha moto akambandikia Johnson maji ya kuoga Johnson akaoga wakaenda bandani wakala chips wakarudi kulala Kesho yake asubuhi, kama kawaida Johnson alienda gengeni kwake akamuacha Maria anajiandaa kwenda nyumbani kwao Johnson alifika gengeni kwake akaanza kufanya usafi akapanga mizigo yake mara akaona gari nyeusi aina ya Noah imepaki mbele ya genge lake alijua labda ni wateja akalifwata lile gari ili awasikiliza kioo kilifunguliwa taratibu Johnson alishtuka hakuamini macho yake alikuwa ni Mama na Baba yake Maria ndio walikuwa kwenye ile gari
Itaendelea......

0 comments:

Post a Comment