SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA....................SEHEMU YA SITA

Ilipoishia
Wazazi wa Maria walitaka kumpeleka Johnson Kituo cha polisi lkn housegirl wao akawapigia simu akawaambia Maria kasharudi nyumbani walifurahi sana wakajadiliana waende na Johnson hadi nyumbani kwao ili wakajue kinachoendelea kati yake yeye na Maria

Endelea
Mama yake Maria yeye hakutaka waendelee kuzunguka na Johnson akamwambia mume wake "Baba Maria mi naona huyu kijana tumshushe ndani ya gari akaendelee na shughuli zake mimi ninavyomuona humu ndani ya gari najiskia hadi kichefuchefu roho inaniuma sana kuona mwanangu anaharibiwa na kimwanaume kama hiki" Johnson alizidi kuumia sana na dharau ambazo mama yake Maria alikuwa anamuonyeshea lakini alivumilia tu sababu yeye ndo alikuwa mwenye makosa kumruhusu Maria alale nyumbani kwake wakati wazazi wake wakali
Baba yake Maria akamjibu "Mke wangu ni vizuri tukaenda na huyu kijana nyumbani tukawahoji vizuri sababu Huyu kijana amekataa amebisha kuwa Maria hakulala nyumbani kwake mimi nataka tukambane Maria vizuri atuambie sehemu aliyolala mbele ya huyu kijana akisema tu alilala kwa huyu bwege nitamfanyia kitu kibaya hatokuja kunisahau"
Wazazi wa Maria wote wakakubaliana waende na Johson nyumbani kwao
Johnson alikuwa ana wasiwasi sana Maria akibanwa anaweza akafunguka kuwa walilala naye akawa anatetemeka sana huku anamuomba mungu amsaidie Maria asimtaje
Walifika nyumbani kwa kina Maria wakaingia ndani Johnson akakalishwa chini tena kwa maneno machafu ya dharau kutoka kwa mama yake Maria aliambiwa "kaa chini we mbwa usije ukanichafulia sofa zangu"
Baba yake Maria alimuita housegirl akamuuliza "huyo mpumbavu yuko wapi?? housegirl akamjibu "yuko chumbani kwake kalala" Housegirl akatumwa akamuamshe Maria haraka sana
Maria alistuka sana kumuona Johnson kaletwa kwao na wazazi wake akabaki anashangaa tu hakuamini macho yake Baba yake akamwambia "unashangaa nn we mjinga kaa hapo utuambie jana umelala wapi na tumemleta huyu bwege wako leo mtueleze vizuri kwanini hamtuelewi kila siku tunavyowaambia muachane"
Maria alikaa kwenye kochi huku anamuangalia Johnson kwa huruma hadi machozi yakaanza kumtoka Baba yake akamwambia "sijakuita hapa uje utulilie nimekuuliza jana tokea asubuhi uage unaenda chuo hujarudi hapa nyumbani ndo unarudi leo tuambie haraka sana ulilala wapi?? Maria hakujibu chochote akabaki tu anamuangalia Johnson huku analia mda huo wote Johnson alikuwa kainama chini huku anamuomba mungu Maria asimtaje kuwa alilala kwake. Baba yake Maria akamuuliza tena kwa ukali "we mpumbavu si nakuuliza jana ulilala wapi sijakuita hapa uje ulie umuangalie huyu mjinga mwenzako"
Johnson aliyainua macho yake yakagongana na ya Maria akamkonyeza Maria ili hata akibanwa asiseme kama alilala kwake Maria akamwambia Baba yake "Baba mimi nalia hapa namuonea huruma huyu kijana wa watu mmeenda kumkamata mmemleta hadi hapa mnamtukana bure tu wakati hana kosa lolote" Baba yake akamuuliza "hana kosa lolote kivipi wakati sisi tunajua huyu bwege ndo anakusumbua akili yako anakufanya usisome anafanya mda wote usikalike hapa nyumbani na kila siku tunakuambia uachane naye lakini husikii"
Maria akamwambia baba yake "Baba huyu kijana hana kosa lolote mnamuonea bure tu mimi sijaonana naye mda mrefu sana nilishaachana naye mda mrefu sina mahusiano naye" Maria alimtetea Johnson hadi wazazi wake wakatulia wakaanza kumuamini Johnson alifurahi sana kuona Maria anamuokoa kwenye ule msala Sababu alijua siku ile ndio mwisho wake anaenda kuozea jela. Mama yake Maria mda wote huo alikuwa kanyamaza kimya huku anamuangalia Johnson juu mpaka chini kwa hasira na dharau akamgeukia Maria akamuambia "we mtoto sisi ni wazazi wako ndio tumekuzaa usitake kutudanganya hapa ukitaka tumuachie huyu mpumbavu tuambie jana ulilala wapi"
Maria akajifikiria akapata cha kudanganya akamjibu mama yake "Mama huyu kijana hana kosa lolote bora mumuache tu aende zake mimi sijalala kwake jana mimi nilitoka chuo na rafiki zangu tukaenda kwenye party nilivyoona kumekuwa usiku sana nikaogopa kurudi nyumbani na nilishindwa kuwapigia simu sababu simu yangu ilikuwa haina chaji nikaenda kulala hostel kwa rafiki zangu ukweli ndio huo mimi sijalala kwa Johnson"
Wazazi wake walimsikiliza Maria kwa makini alivyomaliza kuongea wakaangaliana Baba yake Maria akamwambia "We mtoto siku hizi unajifanya umekua sana hadi umefikia hatua ya kulala nje sasa mimi naongea hapa mbele ya huyu bwege wako nikija tena kukuona umechelewa kurudi nyumbani au hujalala hapa nyumbani au nikija kukuona na huyu kijana utanijua mimi ni nani na huyu bwege wako nitamfanyia kitu kibaya sana" Maria akamwambia baba yake "sawa baba nimekusikia naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea ila mimi huyu Johson niliachana naye mda mrefu sana"
Baba yake Maria akamwambia Jonson "wewe kijana kama unayapenda maisha yako tunakuomba uachane na binti yetu nikija kusikia bado mna mahusiano nitakupoteza" Johson akamjibu" sawa mzee nimekuelewa"
Waliwapiga sana mkwara Johnson na Maria walivyomaliza wakamruhusu Johnson aondoke
Johnson hakuamini macho yake kama amepona kwenye ule msala hakutaka hata kwenda gengeni kwake tena alienda kwake akaoga akalala huku akiapa kutokuwa na mahusiano ya kimapenzi na Maria tena wakati anawaza hivyo simu yake ikawa inaita kuangalia alikuwa Maria

Itaendelea

0 comments:

Post a Comment