Mtunzi: Cox Dawa Yao
Ilipoishia
Johnson alirudi kazini saa 4 usiku akakuta
anapowekaga funguo yake haipo alijiuliza maswali mengi sana aliposukuma
mlango wake akakuta umefungwa kwa ndani akazidi kuchanganyikiwa alianza
kugonga kwa hasira akasikia sauti ya Maria ndani inamkaribisha
Endelea
Johnson aliugonga ule
mlango kwa nguvu akasikia sauti ya Maria ndani inamwambia "bby nakuja
kukufungulia" Johnson akaguna ile sauti ndo ikamchanganya kabisa
hakuamini kabisa kuwa Maria kaja nyumbani kwake usiku wote ule wakati
siku chache tu zilizopota alilala naye kwake wazazi wake wakamletea
balaa,
Maria alifungua mlango akamkumbatia Johnson lakini hata
hakumfurahia akamsukuma akamuuliza "we Maria kwanini hadi muda huu upo
hapa wakati juzi tu umelala huku wazazi wako wakaja kunikamata? Maria
akamjibu "mbona unapanic mpenzi wangu punguza hasira nikueleweshe kaa
hapa kitandani nikuambie kwanini nimejiamini hadi nimekuja usiku wote
huu huku kwako." Johnson alikasirika sana Maria alivyomwambia vile
akatua mzigo wake aliokuwa ameubeba akakaa kitandani amsikilize Maria
anachotaka kumuambia. Maria akamuambia "baby usikasirike mpenzi wangu
kuniona niko huku kwako hadi mda huu Baba na Mama tangu jana hawapo
nyumbani wameenda kwenye msiba Morogoro pale nyumbani tumebaki
mimi,housegirl pamoja na mlinzi wa getini mimi nimeshindwa kuvumilia
sijaonana na wewe siku mbili nimembembeleza mlinzi nimempa pesa
kaniruhusu nitoke ndo nimekuja huku kwako kwa hiyo hata usiwe na
wasiwasi mpenzi wangu"
Johnson alimsikiliza Maria kwa makini
akamuuliza "we unajuaje kama wazazi wako wamempa mtu kazi ya
kukufuatilia itakuwaje umempa mlinzi wenu hela housegirl wenu akibanwa
akiongea kuwa wewe hujalala pale kwenu itakuwaje? Maria akamjibu
"housegirl wetu hawezi kufanya kitu kama hicho bby mimi na housegirl
tunaiva sana na yeye pia nimeshaongea naye"
Johnson kusikia yale
maneno hasira zote zikamuishia akalainika akamwambia Maria "lakini Maria
kuwa makini sana wazazi wako wanapajua hapa kwangu saivi wanaweza
wakarudi mda wowote wakakuta wewe haupo wakija huku wakikukuta sijui
itakuwaje"
Maria akamwambia "usiwe na wasiwasi mpenzi wangu
wanavyorudi najua lazima wapige simu nyumbani mimi nimempigia mama simu
leo kaniambia wanarudi kesho kutwa"
Kusikia vile kidogo wasiwasi wa
Johnson ukapungua Maria akampashia Johnson maji ya kuoga Johnson akaoga
Maria alikuwa amempikia Johnson chakula kizuri akamtengenezea na Juice
Johnson alifurahia sana kile chakula alichopikiwa na mpenzi wake wakala
pamoja wakapiga stori hadi muda wa kulala ulipofika. Usiku ule walipeana
mapenzi motomoto kama ndo mara ya kwanza wanaonana kila mmoja alimmisi
mwenzake sababu toka waanze mapenzi yao hawakuwahi kupitisha siku mbili
bila hawajaonana kwa hiyo walipeana mambo mazito sana ile siku.
Asubuhi kama kawaida Johnson aliwahi kuamka akaanza kujiandaa kwa ajili
ya kwenda gengeni kwake, akamuuliza Maria "baby kwa hiyo wewe unaondoka
saa ngapi? Maria akamjibu "mimi leo siendi chuo nalala hapa hadi mchana
ndio naenda nyumbani kuangalia kinachoendelea" Johson akamwambia "mimi
naondoka nakuomba uwahi kwenda kwenu wazazi wako wasije wakarudi ghafla
wakukose"
Itaendelea
0 comments:
Post a Comment