Mtunzi: Cox Dawa Yao
Simulizi: Johnson Na Maria
Sehemu: Ya Kwanza
Maria alikuwa ni binti wa miaka 21 alikuwa ni mrembo mwenye sifa zote
wanaume wengi sana walikuwa wanamnyemelea lakini yeye alikuwa
anawazingua, alikuwa na boyfriend wake mmoja tu anaitwa Johnsom huyo
ndio mwanaume wake wa kwanza tangu wanasoma
Maria alikuwa anasoma
chuo kimoja huko posta Johson. Johnson matokeo yake yalivyotoka vibaya
sababu kwao walikuwa hawana uwezo alijifungulia genge akawa anauza vitu
vidogovidogo akawa anapata pesa kidgo za kufanyia mambo yake japo
Johnson alikuwa hana kitu ila Maria alimpenda sana na kumuheshimu mara
nyingi sana alikuwa akitoka chuo anampitia Johnson pale gengeni kwake
wanakaa hadi muda wa kufunga
Wazazi wa Maria walikuwa wanakasirishwa sana na
kitendo cha binti yao kumpenda mwanaume masikini kama yule mara kwa mara
walimuonya lakini Maria alikuwa hasikii haoni kwa Johson, mara nyingi
wazazi wake Maria walimfwata Johnson na kumtishia maisha huku
wakimuambia aachane na binti yao hana hadhi ya kutembea na mtoto wao.
Kuna muda Johnson alikuwa anamuambia Maria waachane atafuta mtu mwenye
hadhi kama yake lakini Maria aligoma na alisema "Johnson mimi siji
kukuacha mpaka nakufa na siku ukiniacha mimi nitajiua bora nife kuliko
nikukose"
Kuna siku moja Maria alimfwata Johnson gengeni kwake
hakumkuta, alimfwata nyumbani kwao pia hakumkuta alipopiga simu yake
ikawa haipatikani Maria alichanganyikiwa sana sababu haikuwa kawaida ya
Johnson kwenda sehemu au kuzima simu bila kumuambia
Maria alikaa
pale nyumbani kwa kina Johson hadi saa 4 usiku lakini Johnson hakutokea
Maria alilia sana ile siku alikosa raha kabisa
Itaendelea.....
0 comments:
Post a Comment