Ilipoishia
Wakati tupo kwenye Gari na bro anaenda kunionyesha sehemu ya kazi nilikuwa nachungulia dirishani niliona warembo wa kila aina na masharobaro kibao wakati kwetu nilipotoka walikuwa adimu sana
Wakati tupo kwenye Gari na bro anaenda kunionyesha sehemu ya kazi nilikuwa nachungulia dirishani niliona warembo wa kila aina na masharobaro kibao wakati kwetu nilipotoka walikuwa adimu sana
Nikaanza kuamini maneno ya watu niliyokuwa nayasikia kuwa jiji la Dar es salaam lina kila aina ya watu na lina mambo mengi sana, kaka yangu alikuwa ananielekeza kila jina la kituo gari lilipokuwa linasimama ila mimi nilikuwa natamani sana nipajue kariakoo na Mliman city sababu kuna rafiki zangu walikuwa wananisimulia sana stori ya hizo sehemu nikapanga lazima siku nimuombe bro akanitembeze na mimi nikayaone hayo maeneo. Tulifika kwenye mataa gari likasimama kwenye foleni kaka yangu akaniambia "Dogo ndo tazara sisi tunashukia kituo kinachofuata kinaitwa Buguruni sheli hicho hapo ndio kiwanda cha Azam (Bakhresa) kama ulikuwaga unakisikia basi ndio hicho hapo)
Nilifurahi sana kukiona kile kiwanda cha Azam sababu nilikuwaga naona tu bidhaa zao kiwanda hata nilikuwa sijui kilipo, gari lilisimama kituo kilichofuata mimi na kaka yangu tukashuka bro akaniambia "mdogo wangu hapa ndio Buguruni sheli si unaona watu walivyo wengi hapa kuna mambo ya ajabu sana unatakiwa kuwa makini sana hapa kuna kila aina ya mtu kuna wezi wa mifukoni, wakabaji, madada poa ndio wengi sana hapa pia hii sehemu ina mateja wengi sana unatakiwa kuwa makini sana"
Nilimsikiliza braza kwa makini yale maneno yake yaliniogopesha kidogo sababu kweli niliona mchanganyiko wa watu wengi sana na ilikuwa ni saa nne asubuhi nikawa najiuliza kama asubuhi tu kuna watu wengi vile je jioni itakuwaje. Nikamuambia "nimekuelewa kaka nitakuwa makini sana"
Tulitembea na braza huku njiani akijaribu kunielekeza mambo kibao na kunionyesha baadhi ya sehemu hadi tulifika sehemu lilipo Duka lake hapo mwili wangu ulikuwa unatokwa na jasho balaa sababu ya joto la Dar nilishazoea baridi ya mbeya joto lilinipa sana shida.
Kaka akaniambia "mdogo wangu hili ndio duka langu la hapa Buguruni ambalo wewe utakuwa unauza mimi nitakuwa nashinda kwenye duka langu lingine lipo Kariakoo nakuomba sana uwe makini mdogo wangu kama nilivyokuambia usifanye mchezo na biashara pia angalia watu wa kuzoeana nao hapa kuna wezi,matapeli, kuna watu wajanja sana ukizubaa tu umeumia kuwa makini sana na biashara mdogo wangu"
Nikamjibu "sawa kaka yangu nimekuelewa nitakuwa makini sana nilishazikiaga sana habari za hapa Dar nitajitahidi kufanya biashara kwa nguvu zote kaka sitafanya kabisa mambo ya ajabu"
Kaka yangu akaniambia "nafurahi sana kusikia hivyo mdogo wangu hizi siku mbili nitashinda na wewe hapa Dukani kukuelekeza ili ujue kila kitu ndio nitaanza kukuacha peke yako"
Ile siku tulikaa na braza pale dukani akawa ananielekeza bei za kuuza Cd, bei ya kukodisha Cd, jinsi ya kuwaingizia watu nyimbo kwenye simu na mambo mengine mengi na baadhi ya wateja waliokuwa wanakuja pale dukani alikuwa ananiambia sifa zao. Nakumbuka kuna jamaa alikuja pale kukodi Cd alivyoondoka tu braza akaniambia "dogo umemuona huyo jamaa alitoka hapa sasa hivi akija hapa kuwa muangalifu sana ana tabia za udokozi yani anaweza akaja hapa kuazima Cd anaanza kukupigisha stori kibao ili ujisahau ukizubaa tu au ukimuacha hapa dakika moja lazima aondoke na kitu kuwa naye makini sana"
Nikamjibu "sawa kaka mimi nimeshamuona akija hapa nitakuwa makini sana"
Tulikaa na braza pale dukani tuliagiza chakula tukawa tunakula huku tunapiga stori
Mara kuna wadada wawili wakaja pale dukani wakasalimiana na braza
Mmoja akamuuliza braza "Jose huyo nani tena mbona tunaona sura ngeni?
Braza akawajibu "huyo mdogo wangu anaitwa Cox ametokea Mbeya"
Yule mdada akaniangalia akamuambia kaka "mdogo wako Handsome kama wewe tena amekuzidi hadi wewe"
Kusikia vile wote tukacheka mimi nikajua utani tu wale wadada wanataniana na braza
Itaendelea...................
0 comments:
Post a Comment