SIMULIZI: SITASAHAU NILIVYOOPOA CHANGUDOA JINI...............SEHEMU YA NNE

Ilipoishia
Tulikaa sebuleni na braza tukawa tunapiga stori pale pale na mimi nikaingizia swali langu

Nikamuuliza braza "halafu kaka wakati tupo kwenye gari pale Buguruni nimeona kuna wadada wengi wamevaa vinguo vifupi wengine wanavuta sigara wengine wameshika bia wanafanya nini pale usiku wote ule?
Braza akacheka akanijibu "dogo wale wadada uliowaona pale wote wanajiuza wanatafuta wanaume wa kafanya nao mapenzi ili wapate pesa"
Nikaguna "sasa kaka wewe si uliniambia pale buguruni kuna wakabaji, mateja, wezi wale wadada hawawaogopi?
Braza "wale wadada hawawaogopi sababu wanajuana nao na baadhi ya wadada wanaojiuza pale wanashirikiana na hao watu kuwaibia wanaume"
Nikaguna nikamuuliza "wanashirikiana nao kivipi?
Braza "unaweza ukaenda pale kununua mwanamke akakukubalia mkaenda guest mfano umelewa anawapigia vibaka simu wanakuja kukuibia kila kitu au wanawake wengine ukimchukua anacheza dili na vibaka anawaelekeza mahali mlipo wanakuja kukuvamia wanajifanya wamekufumania na mke wao wale wadada ni watu wabaya sana waone vile vile wengi wao pale ni wezi balaa"
Niliogopa sana kusikia zile habari kutoka kwa braza nikajisemea kweli Dar es salaam kuna mambo
Nikamwambia braza "Basi ile sehemu sio nzuri kaka mimi nimeshangaa sana kuona wanawake wanavuta sigara na wamevaa vinguo vya ajabu hata hawaogopi watu ndio maana nikaona nikuulize ili nijue"
Braza "ndio hivyo mdogo wangu hapa Dar hapafai inatakiwa uwe makini sana ukicheza tu na hili jiji umeumia"
Tulipiga stori na braza pale sebuleni hadi muda wa kulala ukafika wote tukaenda kulala, asubuhi kaka yangu aliwahi kuniamsha kwa ajili ya kwenda kazini niliamka nikaoga nikajiandaa haraka haraka safari ikaanza.
Kama kawaida kwenye daladala nilikaa siti ya dirishani ili niendelee kulijua jiji vizuri na braza pia aliendelea kunielekeza maeneo nikajikuta taratibu hata majina ya vituo nimeanza kuyashika kichwani, japo ilikuwa ni asubuhi lakini nikawa nawaona warembo wazuri wamependeza lakini kwa habari mbaya alizonipa braza kuhusu wanawake wa Dar nikajikuta hata siwatamani nikawa najua kila mwanamke ana tabia za ajabu kutokana na vitisho alivyokuwa ananipa kaka yangu. Gari lilifika pale Buguruni sheli tukashuka na braza nikajaribu kucheki pale nilipowaona wale wadada usiku sikuwaona tena yani kulikuwa na watu wengine wanafanya biashara zao ile sehemu nikajikuta nacheka mwenyewe.
Braza "dogo unacheka nini?
Nikamjibu "nashangaa nimecheki pale nilipowaona wale wadada ulioniambia wanajiuza nimeona watu wamepanga bidhaa zao wanafanya biashara ndio maana nimecheka"
Braza "ndio hivyo dogo pale ukipita asubuhi au mchana huwezi amini kama usiku kunakuwaga na mambo ya ajabu mdua huu watu wanafanya biashara zao usiku machangudoa wanajiuza"
Nikajikuta natikisa kichwa sababu yale mambo kijijini kwetu hayakuwepo kabisa nilikuwaga nasikia tu. Tulifika Dukani tukafungua duka mimi nikawa nafanya usafi braza akawa anapanga vitu
Braza "dogo wewe una kichwa chepesi sana naona siku moja tu umeshazijua bei za vitu na mambo mengine sasa mimi leo nitaenda kucheki Duka langu la kariakoo nitakuacha mwenyewe kuwa makini sana dogo kama kitu hukielewi nipigie simu nikuelekeze"
Nikamjibu "sawa kaka nimekuelewa"
Ulifika muda braza akajiandaa akaondoka zake nikabaki peke yangu

Itaendelea.................

0 comments:

Post a Comment