Mtunzi: Cox Dawa Yao
Ilipoishia
Ilipoishia
Nikajisemea Afadhali nilimpigia braza simu
ningekurupuka tu kutoa hela za dukani kununua ile simu ingekula kwangu
Endelea
Endelea
Nilikaa pale dukani nikasema kweli Dar es salaam pesa zinatafutwa kwa njia nyingi, nilikaa siku mbili tu lakini mambo niliyokuwa nayaona na niliyokuwa naambiwa yaliniogopesha sana. Kila mteja ambaye alikuja pale dukani nilikuwa naye makini sana sikuangalia huyu mtoto,mzee, wote nilikuwa nao makini sana kutokana na mambo niliyoambiwa na braza na ambayo tayari nilikuwa nimeshaanza kuyaona. Nilikaa pale dukani nakumbuka ilikuwa kama mida ya saa nane nilikuwa napata chakula cha mchana wale wadada wawili ambao walikuja kuazima Cd jana yake wakanikuta na braza wakaanza kunisifia walikuja tena pale dukani
Nikasalimiana nao mmoja akaniuliza "Kaka yako yuko wapi wangu?
Nikamjibu "kaka katoka kaenda kariakoo"
Akaguna akaniuliza "yani umekuja juzi tu ameshaanza kukuacha peke yako hapa dukani umeshajua kila kitu?
Nikamjibu "mimi nina kichwa chepesi sana dada yangu yani najua kila kitu hapa"
Akaniuliza "hivi jina lako nani sababu hata jina hatukujui?
Nikamjibu "mimi naitwa Coxian ukipenda unaweza ukaniita Cox"
Akaniambia "jina lako zuri sana wangu unaendana nalo kabisa"
Nikacheka nikamuuliza "yani naendana nalo kivipi mbona sijakuelewa dada?
Akanijibu "kwani wewe hujioni ulivyo wewe ni Handsome sana una mvuto na jina lako zuri sana ndio maana nimekuambia unaendana nalo"
Nikamwambia "mbona mimi wa kawaida tu dada yangu yani wewe ndio mtu wa kwanza kunipa sifa kama hizo"
Akaniambia "Acha uongo bhana basi ambao hawakuambii wanakuonea wivu"
Yale maneno ya yule dada yalinifanya nicheke mwenyewe lakini nikakumbuka kauli ya braza aliyoniambia kuwa wasichana wa mjini ni wajanja sana wana njia nyingi za kumtapeli mtu kwa hiyo na mimi pale nikajua yule dada ananisifia kuna kitu anakitaka. Muda wote naongea na yule mdada mmoja yule mwengine alikuwa bize anachezea simu yake, nilivyoona stori nyingi alafu hawaniambii shida yao nikaamua kuwauliza sababu nilijua braza akinikuta pale dukani napiga stori na wale wadada atanifikiria vibaya.
Nikawauliza "niwasaidie nini dada zangu naona tumenogewa na stori"
Mmoja akanijibu "sisi tumekuja kurudisha zile Cd tulizoazima jana halafu tunataka nyingine ila tumefurahi sana kukuta wewe hapa ndio maana tumenogewa na stori"
Nikawajibu "hata mimi nimefurahi sana kupiga stori na nyie dada zangu niwape Cd gani jamani"
Wakaanza kujadiliana wenyewe pale wakacheki cheki pale wakaniambia "Tunaomba cd ya kibongo inaitwa Sikitiko Langu tumesikia ni nzuri sana"
Walivyoniambia tu nilianza kuitafuta hyo cd hadi nikaipata, nikawapa ile Cd nikashangaa kuona mmoja katoka nje akabaki yule mwengine ambaye alikuwa ananisifia sana hadi nikaanza kuogopa nikajua wale wadada kuna kitu wamepanga.
Nikamuuliza "mbona rafiki yako anakuacha?
Akaniangalia akatabasamu akaniambia "yani mimi natamani hata nisiondoke tumepiga stori kidogo tu tayari nimeshakuzoea"
Nikamuambia "hata mimi nimefurahi sana kupiga stori na nyie wenyeji wangu ila usijali siku nyingine tena muda ukipatikana tutapiga stori sana tu si unajua hii mida ya kazi dada"
Nilimuambia hivyo ili aondoke pale dukani sikutaka kabisa braza amkute pale na pia sikupenda watu wa yale maeneo wanione nimeanza kuzoeana na wanawake wajue nna tabia mbaya.
Yule dada akaniambia "kweli hii mida ya kazi
wangu nipe namba yako ya simu basi tuwe tunawasiliana"
Nilishangaa sana kusikia yule dada anitaka namba yangu ya simu nikawa nasita kumtajia sababu sikujua lengo lake ni nini
Itaendelea.....................
Nilishangaa sana kusikia yule dada anitaka namba yangu ya simu nikawa nasita kumtajia sababu sikujua lengo lake ni nini
Itaendelea.....................
0 comments:
Post a Comment