SIMULIZI: SITASAHAU NILIVYOOPOA CHANGUDOA JINI............SEHEMU YA SABA

Mtunzi: Cox Dawa Yao
Ilipoishia
Nilishangaa sana kuona yule dada anaitaka namba yangu nilisita kumpa sababu sikujua lengo lake ni nini
Endelea

Yule dada alivyoongelea swala la namba ya simu mimi nikawa napotezea nikawa najifanya nipo bize napangapanga vitu pale dukani, Alivyoona napotea akaniambia "Coxian jamani naomba basi unipe namba yako mimi nataka kuondoka rafiki yangu ananisubiri"
Nikamuambia "nitakupa siku nyingine wangu sio leo"
Akaniuliza "kwanini usinipe leo wangu?
Nikamjibu "simu yangu kuna mtu nataka kumpa kwa hIyo sitakuwa hewani hata nikikupa itakuwa kazi bure tu"
Akaguna akaniambia "we nipe hivyo hivyo ukiwa hewani tutawasiliana au hutaki tuwe tunachati Cox jamani"
Nikamwambia "hamna wangu sio hivyo mimi kweli sitakuwa hewani ila ngoja nikupe tu uwe nayo"
Nilivyoona yule dada anang'ang'ania sana namba yangu nikaamua kumpa namba yangu ya voda ambayo hata nilikuwa siitumii mara kwa mara
Alifurahi sana nilivyomtajia namba lakini alijaribu kupiga palepale akakuta namba haipatikani
Akaniuliza "Cox mbona umenipa namba napiga haipatikani?
Nikamjibu "hiyo ndio namba yangu ila simu yangu nimeichaji ndio maana haipatikani"
Nilivyomjibu vile akaniambia "basi poa wangu mimi ngoja niende nitakupigia baadae tuongee"
Kilichonishangaza yule dada anavyoondoka aliniangalia akanichekea akaniaga kwa busu la mbali, pale ndo nikaanza kuyaamini yale maneno ya braza aliyoniambia kuwa wanawake wa mjini wajanja sana wakimtaka mwanaume wanampata kwa mbinu yoyote. Niliendelea na shughuli zangu pale dukani lakini bado tu nikawa nawafikiria wale wadada yani siku mbili tu nimekaa pale dukani wameshaanza kuniletea mambo kama yale nikawa najiuliza sijui sasa huko mbele itakuwaje.
Jioni ilifika braza akanipitia pale dukani akaniuliza "vipi mdogo wangu biashara zinakwendaje haujasumbuliwa?
Nikamjibu "hakuna aliyenisumbua braza zaidi ya yule jamaa aliyetaka kunitapeli kwa njia ya kuniuzia simu"
Braza akaniambia "afadhali ulinipigia simu mdogo wangu umefanya vizuri sana ungekurupuka tu kumpa pesa tungeingiliwa leo"
Braza alinisifia sana kuwa nipo makini lakini sikumuambia kuwa wale wadada walikuja pale dukani nikajua lazima ataanza maswali sababu siku ya kwanza walinishobokea mbele yake. Tulianza kufunga duka pale braza akaniambia "mdogo wangu leo tunafunga duka hapa tunaenda zetu Sinza nikakutembeze kidogo viwanja ulione jiji la Dar es salaam linavyochanganya"
Nilifurahi sana kusikia vile sababu nilikuwa natamani sana siku na mimi nizurure usiku nione jiji linavyokuwa sababu nilikuwaga nasimuliwa sana stori kuwa Dar es salaam usiku ni kama mchana watu wanakula sana raha. Tulipanda Bajaji na braza akaniambia "mdogo wangu tunaenda sehemu moja inaitwa Soccer City napapenda sana pale pametulia sana"
Nikamjibu "sawa kaka mimi nakusikiliza wewe najua kama wewe umepapenda lazima tu patakuwa pazuri"
Kama kawaida yangu wakati tupo njiani mimi nilikuwa nashangaa shangaa jiji lilivyo na braza alikuwa ananielekeza baadhi ya maeneo hadi tukafika mwisho wa safari yetu, tulishuka ndani ya bajaji tukaingia pale tukaangalia meza ambayo haina watu tukakaa.
Braza akaagiza chakula tukala yeye akawa anakunywa Bia mimi nikawa nakunywa juice nilikuwa situmii pombe kabisa, kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda watu walizidi kuwa wengi na wanawake ndio walikuwa wengi sana. Kulikuwa na warembo wa kila aina mimi nikawa tu nawashangaa asilimia kubwa walivaa nguo za kuonyesha mapaja yao maziwa yao wengine walivaa nguo zinazoonyesha nguo zao za ndani na shanga walizovaa kiunoni. Niliona ajabu sana sababu sikuzoea kuona mambo kama yale nikajisemea kweli jiji la Dar es salaam limechafuka

Itaendelea...........

0 comments:

Post a Comment