Mtunzi: Cox Dawa Yao
Ilipoishia
Niliendelea kushangaa wadada walivyovaa vinguo vya kuonyesha mapaja na maziwa yao nikasema kweli Dar se salaam imechafuka
Endelea
Kwenye ile meza tuliyokuwa tumekaa na braza kuna wadada
kama watatu walikuja pale, wakatusalimia tukaitikia mmoja akatuuliza
"samahanini wakina kaka tunaweza kukaa na nyie hapa?Niliendelea kushangaa wadada walivyovaa vinguo vya kuonyesha mapaja na maziwa yao nikasema kweli Dar se salaam imechafuka
Endelea
Braza akamjibu "hapana dada kuna wageni wetu tunawasubiri wapo njiani wanakuja watakaa hapa"
Braza alivyowajibu vile wale wadada wakakaa meza ya pembeni yetu na wenyewe pia walikuwa wamevaa vinguo vifupi mmoja alikuwa anavuta sigara nikajua tu na wenyewe watakuwa wanajiuza ndio maana braza hakutaka tukae nao meza moja. Kati ya wale wadada kuna mmoja alikuwa ananiangalia sana hadi nikawa nahisi atakuwa amewahi kuniona sehemu sababu macho yetu yalikuwa yakigongana akawa ananichekea.
Braza akaniuliza "Dogo vipi mbona unawacheki sana hao wadada?
Nikamjibu "kuna mmoja ananitolea sana macho braza sijui ananifananisha"
Braza akaniambia "hamna mdogo wangu hakufananishi wala nini hao wadada ni machangudoa wanajiuza hapa usiwaone wamependeza hivyo wamekaa wenyewe wanakunywa hapo wametega mwanaume yoyote ukijipendekeza unaondoka nao ndio maana walivyoomba kukaa na sisi hapa mimi nikawadanganya kuna watu wanakuja kukaa"
Mimi nikaguna nikamuambia "yani hao wadada wangejiona jinsi walivyo wasingethubutu kufanya biashara ya kuuza miili yao wadada wazuri hao wangetulia hata hawawezi kukosa waume wa kuwaoa"
Braza akaniambia "ndio hivyo mdogo wangu maisha magumu ndio yanafanya mpaka wajiingize kwenye hiyo biashara japo wengine ni mazoea tu"
Nikamuambia "hao wadada ni wavivu tu wanapenda kujipatia pesa kwa njia rahisi mbona kazi za kufanya zipo nyingi tu kwani lazima wauze miili yao"
Braza akaniambia "ndio hivyo mdogo wangu hii ndo Dar es salaam usije ukathubutu kuchukua wanawake wa aina hiyo unaweza ukajipatia magonjwa ya ajabu alafu pia kuna baadhi yao wana tabia mbaya sana ukikaa nao meza moja mnakunywa ukizubaa tu lazima wakutilie dawa za kulevya kwenye kinywaji chako ukinywa zikikulevya wanakuibia kila kitu"
Braza alivyokuwa ananielezea tabia za wale wadada nilizidi kuwaogopa nikasema kweli jiji la Dar lina mengi
, kadri mda ulivyokuwa unazidi kwenda ndo idadi ya wanawake ilikuwa inazidi kuongezeka. Nilikuwa nawaona wengine mwanaume akipita wanamuita mara wamvute pale ndo nikapata uhakika wanawake wengi waliokuwepo pale walikuwa wanajiuza.
Braza aliniambia "dogo ngoja mimi nikacheze mziki kidogo hii nyimbo inayopigwa naipenda sana"
Braza alisimama akaenda kucheza mziki akaniacha mimi pale mezani naendelea kunywa soda yangu na kushangaa mazingira. Yule mdada aliyekuwa ananiangalia sana nikaona kasimama pale alipokuwa amekaa akanifuata mimi pale mezani kwetu, akavuta kiti akakaa karibu na mimi sikujua kafuata kitu gani mimi nikatulia tu nikawa nasubiri kusikia anachotaka kuniambia. Yule dada akaniambia "kaka samahani kwa usumbufu naomba niagizie bia kama hutojali"
Nikamjibu "mimi hapa sina hela dada yangu nimekuja na kaka yangu ndio anasimamia kila kitu"
Yule mdada akaguna akaniambia "mbona muonekano wako unaonyesha wewe ni mtu ambaye huna shida najua tu unaninyima
Nikamuambia "sio hivyo dada mimi sina kitu alafu naomba uondoke hapa kaka yangu akinikuta naongea na wewe hapa itakuwa kesi"
Yule mdada akaniambia "yani wewe na ukubwa wote huo bado tu unachungwa kama mtoto"
Nikamjibu "yule ni kaka yangu lazima nimuheshimu ndio maana nakuambia uondoke hapa"
Nilikuwa naongea na yule dada kwa wasiwasi sana nikajua labda kuna kitu anakitaka kutoka kwangu sikuwa na imani naye kabisa.
Itaendelea..........................
0 comments:
Post a Comment