SIMULIZI: SITASAHAU NILIVYOOPOA CHANGUDOA JINI......................SEHEMU YA TISA

Mtunzi: Cox Dawa Yao

Ilipoishia
Nilikuwa naongea na yule mdada kwa wasiwasi sana nikajua kuna kitu anakitaka kutoka kwangu sikuwa na imani naye kabisa
Endelea
Nikamuambia yule mdada "we dada naomba basi uondoke kwenye hii meza mimi nimeshakuambia kaka yangu akikukuta hapa itakuwa balaa"
Akanijibu "Acha uoga wewe mkaka basi naomba unipe namba yako na mimi nikupe yangu siku tukiwa na muda tutafutane"
Nikamjibu "mimi siwezi kukupa namba yangu wakati sikujui kwanza unaitaka namba yangu ya nini"
Yule dada alikuwa anaongea na mimi huku anakinyonga kiuno chake pale kwenye kiti na kile kinguo kifupi alichokivaa hadi nguo yake ya ndani ilionekana mapaja yote yalikuwa yanaonekana. Pale ndio alizidi kunikasirisha braza alikuwa bize anacheza mziki hata sikujua kama amemuona yule dada pale mezani au hajamuona, nilitamani niondoke pale mezani nimuache peke yake lakini niliogopa atatuwekea Dawa kwenye vinywaji vyetu.
Yule dada akaniambia "we mkaka hebu angalia jinsi mtoto ninavyolipa jisachi basi nikakupe mchezo nikakupe mambo matamu"
Pale ndio sikumuelewa nikamuuliza "mbona sikuelewi wewe dada nijisachi kivipi ukanipe mchezo gani"
Akanijibu "we mkaka acha kujifanya hujui kitu wakati wewe unaonekana mtu mzima yani nakuambia twende tukafanye mapenzi mimi kulala nafanya 30000 ukitaka fasta fasta unanipa 10000"
Pale ndio nilimuelewa yule mdada nikatingisha kichwa nikamuambia "sikiliza wewe dada mimi sijaja hapa kununua mwanamke nimekuja kwenye mambo yangu na kaka yangu hebu toka hapa tena koma kabisa mimi sina mambo ya kipumbavu kama hayo"
Nilivyoonyesha ukali na kubadilisha sura kabisa nikajua labda yule dada atatetemeka na kuniogopa, nilishangaa kuona yule dada kaniangalia kwa nyodo juu hadi chini akaniambia "wewe mkaka unaonekana mjanja mtoto wa mjini kumbe lishamba tu yani unakataa kwenda kupewa kitu roho inapenda kaogeeeee"
Yule mdada alivyoongea yale maneno ya kunikashifu akaniangalia tena kwa dharau akaondoka zake akaenda kukaa kwenye meza yao. Nilikasirika sana nilitamani hata nimfuate nimpige lakini nikajizuia sababu nilikuwa bado mgeni yale maeneo na braza alivyoniambiaga wadada wanaojiuza wanajuana sana na wahuni nikajua wanaweza wakanivamia wakanipiga kwa kunichangia na kuniibia na muda ule mauzo yote nilikuwa nayo mimi. Nilikaa pale mezani nakunywa soda yangu huku naendelea kuangalia mambo ya ajabu yanayofanyika yale maeneo, braza alirudi pale mezani akakaa akaniuliza "vipi mdogo wangu umechoka tuondoke zetu?
Nikamjibu "mimi niko freshi braza wala sijachoka ila naona muda umeenda sana bora tuondoke ili kesho tuwahi kazini tusije tukachelewa kuamka na ukicheki wewe umekunywa sana pombe"
Braza akaniambia "poa mdogo wangu malizia basi soda yako na mimi namalizie hii bia fasta tuondoke"
Nikamuambia "mimi niko fresh braza soda zimenijaza sana tumbo malizia bia yako tuondoke"
Braza akaniambia "halafu dogo nimekumbuka muda ule nacheza mziki kule mbele nimemuona mdada kakaa hapa anaongea na wewe alikuwa anakuambia nini?
Nikamjibu "nitakusimulia nyumbani kaka ila hii sehemu uliyonileta siyo nzuri yule dada kanikera sana"
Sikutaka kumuhadithia braza pale pale nilihofia anaweza akaanzisha fujo sababu braza nilimjua alikuwa akilewa anakuwa mtata sana

Itaendelea.......................

0 comments:

Post a Comment