Karibu ulete mataji: Kocha mpya wa Manchester United,
Van Gaal akiwa na Kocha Msaidizi, Ryan Giggs kushoto
Aliwasili na ndege hii binafsi Uwanja wa Ndege wa Manchester
Salamu: Van Gaal (katikati) amekutana na msaidizi wake Ryan Giggs (kushoto) na makamu mwenyekiti Ed Woodward.
KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amewasili katika uwanja wa mazoezi wa Carrington leo jumatano kuanza kazi yake mpya.
Mholanzi
huyo alipigwa picha akiwa geti kubwa, lakini baadaye klabu iliposti
picha katika mtandao wake wa Twita akiwa na msaidizi wake Ryan Giggs na
makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward.
Van Gaal alitaka kuonana na wachezaji wake baada ya kombe la dunia pamoja na viongozi wa klabu hiyo.
Van Gaal amerudi baada ya kuiongoza Uholanzi kushika nafasi ya tatu ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Majadiliano: Giggs, Van Gaal na Clive Woodward wana kibarua kikubwa cha kuirudisha United katika hadhi yake.
Van Gaal ametua kazini siku nne tu tangu aiongoze Uholanzi kushika nafasi ya tatu na kwa maana hiyo amejinyima mapumziko.
Kocha
huyo mwenye miaka 62, ni kocha wa kwanza kuiongoza Man United kutoka
nje ya British,na hatakuwa na muda wa kupoteza katika harakati zake za
kuijengga United.
Kesho
alhamisi, atatangazwa rasmi katika mkutano wake wa kwanza na waandishi
wa habari kabla ya kuanza safari ya kwenda nchini Marekani kuweka kambi
ya maandilizi ya kabla ya msimu.
United
itacheza mechi dhidi ya Los Angeles Galaxy, Roma, Inter Milan na Real
Madrid, wakati mechi ya kwanza ya Van Gaal katika dimba la Old Trafford
itakuwa ya kirafiki dhidi ya Valencia Agosti 12 mwaka huu.
Siku nne baadaye United wataanza ligi kuu kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Swansea.
Watu wa kazi: Giggs (kushoto) na Van Gaal watafanya kazi pamoja kufuta majanga ya David Moyes msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment