KOCHA Louis van Gaal ametua mjini Manchester tayari kuanza kazi katika ofisi mpya, Old Trafford.
Mwalimu
huyo wa Manchester United alitua kwa ndege binafsi Jijini humo majira
ya Saa 2.40 leo asubuhi na moja kwa moja kupelekwa makao makuu ya klabu,
Carrington.
Atasalamiana
na wakuu mbalimbali wa klabu hiyo kabla ya kuzungushwa kwenye Uwanja wa
mazoezi na kisha kutambulishwa kwa wachezaji.
Atakutana na wachezaji: Van Gaal atatambulishwa wachezaji wa timu hiyo Carrington kabla ya kuanza kazi
Atapata fursa ya kuanza kujenga uhusiano na wachezaji baada ya kuongoza mazoezi kidogo kwa mara ya kwanza na
United inatarajiwa kumtambulisha rasmi kwa umma kesho katika Mkutanno na Waandishi wa Habari.
Mara
baada ya kutambulishwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 atapaa tena
na kikosi chake kwenda ziara ya Marekani ambako watacheza mechi nne.
Kocha
huyo wa zamani wa Bayern Munich anaamini hana sababu ya kupumzika kwa
sasa baada ya kuiongoza kwa mara ya mwisho Uholanzi katika Kombe la
Dunia, zaidi ya kuanza kazi kwa mwajiri mpya.
Uholanzi
ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia baada ya
kuwafunga wenyeji, Brazil mabao 3-0 wakitoka kutolewa kwa penalti na
Argentina katika Nusu Fainali.
Likizoni: Robin van Persie amepewa ruhusa ya mapumziko ya wiki tatu kabla ya kurejea kazini Man United
La
Galaxy, Roma, Real Madrid na Inter Milan ndiyo timu ambazo zitamenyana
na United na kumpa Mholanzi huyo fursa ya kukitathmini kikosi chake
kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England baada ya msimu mbaya uliopita
chini ya kocha aliyemtangulia, David Moyes.
Van
Gaal anatarajiwa kuchukua maamuzi zaidi ya kikosi hicho, pamoja na
kuwakaribisha wachezaji wapy, Ander Herrera na Luke Shaw.
Chris
Smalling, Tom Cleverley, Javier Hernandez, Shinji Kagawa, Darren
Fletcher, na Ashley Young wote watasubiri kujua hatima yao kama watabaki
Old Trafford. Robin van Persie yupo kwenye likizo ya wiki tatu baada ya
Kombe la Dunia.
0 comments:
Post a Comment