Waumini wa Kanisa la Anglikana Temeke jana nusura WAZIPIGE wakati wa ibada

Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu Dk Valentino
Mokiwa.Waumini wa Kanisa la Anglikana la Watakatifu wote Temeke, jana
nusura wazipige wakati ibada ikiendelea ambapo hali hiyo ilijitokeza
baada ya kusomewa barua ya utambulisho wa Padri Samweli Kilango ambaye
waumini hawamtaki kwa madai ya ufujaji wa fedha.
Baada ya kusomwa barua hiyo na Katibu wa Kanisa hilo, Hamuli Kapungu, ndipo mtafuruku ukaanza
ambapo mmoja wa waumini alitoka mbele, kuchukua kipaza sauti na kusema
kwa sauti kubwa mbele ya waumini wenzake kuwa hawamtaki mchungaji
huyo.Wakizungumza na Mwandishi kanisani hapo Dar es Salaam jana,
waumini hao walimshangaa Askofu wa Kanisa hilo Jimbo la Dar es Salaam
Valentino Mokiwa wakidai ameshindwa kusikilizamalalamiko ya waumini wa
kanisa hilo kwa sababu mchungaji huyo tayari ameshakataliwa katika
makanisa matatu lakini Askofu anashindwa kuchukua hatua dhidi
yake.Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao, walisema wao
kama waumini wa kanisa hilo, hawamtaki kiongozi huyo kutokana na tabia
zake lakini kubwa zaidi ni mfujaji wa fedha za kanisa.Walisema
mchungaji huyo tayari amekataliwa kwenye Kanisa la Anglikana Buza na
Tabata Kisukuru lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa badala yake
anapewa uhamisho.Waliongeza kuwa, kitendo cha Askofu Mokiwa kushindwa
kusikiliza kero za waumini wake dhidi ya mchungaji huyo, hali hiyo
imesababisha waumini kuhama kanisa hilo na kwenda kusali makanisa
mengine.Chanzo hicho cha habari, kilisema sababu ya Askofu Mokiwa
kufumbia macho tabia za mchungaji huyo ni ukaribu wao hivyo ni vigumu
kumchukulia hatua kama wanavyotaka waumini.Akijibu tuhuma hizo,
Mchungaji Kilango alisema hizo ni mbinu za shetani zinazoingia
makanisani na kama waumini hawawezi kumsikiliza Mungu au kiongozi
waliyemteua inakuwa tatizo.Alisema kwa mujibu wa kanuni za kanisa
hilo, yeye ni mtawala wa kanisa pia ni mchungaji hivyo ni jukumu lake
kuwaongoza waumini bila ubaguzi wa kikabila wala itikadi yoyote."Sina
haja ya kueleza kwanini nimetokaTabata Kisukuru au Buza na anayetaka
kujua kwanini nimetoka huko basi aende kwa Askofu Mokiwa, sihitaji
kutetewa na mtu yeyote wala rafiki kwani Mungu hakunituma kuja kusifia
watu bali kufanya kazi yake,"alisema.Baada ya sakata hilo, Mwandishi
alifanya jitihada za kumtafuta Askofu Mokiwa kwa lengo la kujibu
tuhuma hizo za waumini wa kanisa lake na baada ya kumpata, alisema
hakuwa na taarifa zozote za malalamiko hayo hivyo hawezi kujibu
chochote.

0 comments:

Post a Comment