Bofya hapa
Jiridhishe kwa kutembelea NECTA
Siku hizi hakuna Divisions, na tafsiri ya GPA ni hii hapa kwenye jedwali, Distinction ndio kama Division I ukipenda.
http://www.necta.go.tz/files/utaratibu_wa_kutunuku.pdf
GPA
DISTINCTION | MERIT | CREDIT | PASS | FAIL |
3.6 - 5.0 | 2.6 - 3.5 | 1.6 - 2.5 | 0.3 - 1.5 | 0.0 - 0.2 |
Qualifying Test (QT): Tembelea HAPA
UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA CHA SITA KWA
KUTUMIA MFUMO WA GPA
1. Mfumo wa Wastani wa Pointi (Grade Point Average - GPA)
Huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa katika masomo aliyofaulu katika mtihani wake.
GPA hutokana na masomo saba (07) aliyofaulu vizuri zaidi mtahiniwa katika Mtihani wa Kidato cha Nne na masomo matatu (3) ya tahasusi katika Mtihani wa Kidato cha Sita. Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 07 kwa CSEE au pungufu ya 03 kwa ACSEE, atafaulu katika kiwango cha “Pass” endapo atapata angalau Gredi D katika masomo mawili au gredi C, B, B+ au A katika somo moja.
Uzito wa Gredi A= 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D = 1, E = 0.5 na F = 0.
Utaanza kutumika kupanga madaraja ya ufaulu katika Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2014 na Kidato cha Sita (ACSEE) 2015.
2. Ukokotoaji wa GPA ya Mtahiniwa
Hufanyika kwa kuchukua jumla ya uzito wa gredi katika masomo saba (07) aliofanya vizuri kwa Mtihani wa Kidato cha Nne na matatu (3) ya tahasusi kwa Mtihani wa Kidato cha Sita na kugawanya kwa idadi ya masomo. Ukokotoaji huo huzingatia kanuni ifuatayo:
GPA =
Jumla ya Uzito wa gredi za masomo
------------------------------------------------
Idadi ya Masomo
Masomo yatakayotumika katika ukokotoaji wa GPA ya mtahiniwa ni yale ambayo amefaulu; yaani amepata Gredi A, B+, B, C au D.
3. Muundo wa Madaraja Kwa Kutumia Mfumo wa GPA
Katika mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA) kutakuwa na madaraja manne ambayo ni Distinction, Merit, Credit na Pass.