Aina mpya ya Mauaji ya WasichanaYaibuka Lindi..... Saba wamefariki baada ya kubakwa na kuchomekwa Chupa sehemu zao za Siri


Wasichana saba wamepoteza maisha wilayani Nachingwea mkoani Lindi
baada ya kubakwa na kunyongwa kisha kuwekewa vijiti na chupa kwenye
sehemu zao za siri.Wasichana hao wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti
katika kipindi cha miezi minne iliyopita na wamekuwa wakipigiwa simu
nyakati za usiku na kukutana na waliowapigia simu ambapo hubakwa na
kunyongwa na kisha katika sehemu za siri kuwekewa vijiti au chupa.Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amebainisha aina hiyo ya mauaji
jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika
Hospitali ya Mkoa ya Sokoine.Mwananzila alikuwa amekwenda hospitalini
hapo kuwatazama majeruhi ambapo alifafanua kuwa mauaji hayo
yanaendelea na juzi mtu mwingine aliuawa katika mazingira
hayo.Alisema,"serikali ya wilaya ilishatoanamba za simu kuwa
unapopigiwa simu mtoto wa kike fanya juhudi kumjulisha mwenzako au
piga simukituo cha polisi ili kuweza kukabiliana na watu hao wanaotoa
roho za watu".Mwananzila alisema kuwa binti mmoja aliweza kupigiwa
simu na kundi hilo, aliamua kupiga simu kituo cha polisi na kuweka
mtego baada yeye kutoka nje, polisi walikuwa wameshazingira maeneo
hayo na wauaji wale walimfuata ndipo huyo binti alianza kuvutana nao
na hatimaye Polisi waliwatia mbaroni watu hao.Mkuu huyo wa mkoa
aliwaonya mabinti hao na kusema: "ni makosakwa wasichana kutoka nje
baada ya kupigiwa …"kinachotakiwa kwanza mjulishe mwenzako, lakini
unafanya siri madhara yataweza kukutokea, hususani watoto wa
kike".Alisema mauaji hayo yana ishara ya imani ya kishirikina. Hata
hivyo uchunguzi unaendelea kufanyika.Alisema suala hilo liko ndani ya
uchunguzi hivyo ni vizuri kufanyia kazi kwanza na kuwataka wananchi
wawe na subira.

0 comments:

Post a Comment