Wakili wa Serikali anayekabiliwa nakesi ya kumjeruhi Hausigeli aendelea kusota Rumande

  

Wakili wa Serikali, Yasinta Rwechungula (44) Mkazi wa Boko njia
panda, anayekabiliwa na kesi ya kumpiga na kumjeruhi mfanyakazi wake
wa ndani ameendelea kusota rumande kutokana na kutotimiza masharti
yadhamana.Hakimu wa Mahakama ya Mkazi Kinondoni, Amaria Mushi,
alimtaka kuwa na wadhamini wawili kutoka taasisi inayotambulika
watakaosaini hati ya dhamana ya Sh milioni nne.Alishindwa kutimiza
masharti hayo hivyo alirudishwa rumande hadi Julai 29 mwaka huu kesi
yake itakaposikilizwa.Mwendesha Mashitaka wa Serikali Masin Musa
alidai Juni 11 mwaka huu mshitakiwa alifikishwa katika Mahakama hiyo
kwa kosa la kupiga na kujeruhi mwili.Alidai mshitakiwa alimpiga
msichana wake wa kazi Malina Mathayo (15) kwa kutumia waya wa kompyuta
mwilini na kumpiga na brenda kichwani na kumsababishia majeraha ya
mwili.Pia alidai Juni 17 mwaka huu , Jamhuri waliweka zuio la dhamana
kwa ajili ya usalama wa mtuhumiwa, huku akidai kuwa hali ya mgonjwa
mpaka sasa inaendelea vizuri.Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Mushi
alisema ameridhika na ufafanuzi uliotolewa na MwendeshaMashitaka wa
Serikali Musa pamoja na Wakili wa mshitakiwa Golden Njahara, hivyo
alidai haki yadhamana iko wazi endapo atatimiza masharti yaliyopangwa 

0 comments:

Post a Comment