Mtoto Devota Malole aliyekuwa amelazwa
katika hospitali ya wilaya ya Kilosa kufuatia
mama yake kumtesa kwa kumfungia ndani
na kumlaza chini kwa muda wa miaka
mitano amehamishiwa katika hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Morogoro
baada ya afya
yake kiafya kubadilika.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya
kilosa Dr Shedrack Mponzi amesema
wamelazimika kumuhamishia mtoto huyo
katika hospital ya rufaa ya mkoa wa
Morogoro baada ya hali yake kuwa mbaya
na uchunguzi wa awali umebaini
anamagonjwa mbalimbali ikiwemo utapia
mlo kwa kukosa lishe ambapo katika
hospitali ya mkoa wa morogoro waandishi
wetu wameshuhudia madaktari wakifanya
kila juhudi za vipimo na matibabu.
Wasamaria wema wamejitokeza katika
hospitali ya mkoa wa Morogoro kumjulia
hali mtoto Devota ambapo mbunge wa
jimbo la Morogoro Abdul Azizi Abood
amewataka maafisa ustawi wa jamii
kuacha kulala na badala yake watekeleze
wajibu wao ipasavyo kuwasaidia watoto
wanaoteseka .
Nae mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi
ya Alsaidi Omari Alsaidy ameahidi
kugharamia matibabu ya mtoto huyo hata
kama italazimika kupelekwa nje ya nchi
kwa matibabu ili kunusuru maisha yake.
0 comments:
Post a Comment