Kajala amvaa tena Wema Sepetu......Asema ni MNAFIKI na Kigeugeu

Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kusema kuwa
ushosti wake na Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu, uliorudishwa hivi
karibuni baada ya kuwekana sawa ni wa kinafiki huku akidai Wema ni
kigeugeu.Akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, juzi
Jumatano pande wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala alisema:
"Wema ni mnafiki kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi moyoni
nimeondoakinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge
moyoni."Kajala alisema hayo alipoulizwa na Risasi Jumamosi, sababu ya
kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama
mzazi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond', Sanura Kassim ambaye ni
mkwe wa shosti wake huyo.Katika tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa
sapraizi ya nguvu alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota Lexus
Harrier kama zawadi ya bethidei yake, ambayo ilitolewa na meneja wa
Diamond, Babu Tale kwa niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa
safarini nchini Marekani."Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini
mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha
kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona
amealika watuwengi lakini mimi ameniacha? Wema aache unafiki
bwana."Mbaya zaidi, hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja
anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi kugomabana naye,
lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya
kumsifia akim-wish happy birthday,hapo si kama ananisimanga? Wema si
mkweli,"alisema Kajala.Akizungumzia ishu hiyo, siku ya tukio Wema
alisema:"Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa
kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana."Hata
ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita
Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili)
usiku tu,"alisema Wema

0 comments:

Post a Comment