Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini aahidi kuwakamata walipuaji mabomu Arusha

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amesema jeshi hilo
lina uhakika wa kuwapata watuhumiwa wa mabomu mkoani Arusha na
kwingineko nchini, pamoja na kudhibiti matukio hayo baada ya
kukamilika kwa uchunguzi wa taarifa walizopata.Mangu alisema hayo jana
wakati wa mkutano baina yake na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia,
LuteniJenerali Sebastian Ndeitunga ambaye ni Mwenyekiti wa Shirikisho
la Wakuu wa Polisi kusinimwa Afrika (SARPCCO).Akijibu swali la
waandishi wa habari kuhusu milipuko ya mabomuya Arusha na hali ya
usalama nchinikwa sasa, Mangu alisema hali ya usalama siyo ya kutisha
kutokana na matukio hayo mapya na ambayohayajazoeleka nchini."Kila
tukio lina sababu zake hivyo wanaendelea na uchunguzi wa taarifa
walizopata ambazo wanazifanyia kazi na kuna uhakika wa kukabiliana na
matukio hayo kwa kuwapata wahalifu na kuyadhibiti kabisa,"alisema
IGP.Huku akiwataka wananchi kushirikiana na polisi kuhakikisha
wanafikia malengo hayo mapema kutokana na ukweli kuwa kuna wananchi
wanafahamu mipango hiyo na wanaojihusisha, kwani wapo kwenye jamii
lakini wako kimya.Wakati Mangu anaeleza hayo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
MagesaMulongo, amewataka wananchi, viongozi wa taasisi mbalimbali za
kijamii, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na viongozi wa dini
kushirikiana na serikali ili kuharakisha kasi ya kuwapata
watuwanaojihusisha na ulipuaji wa mabomu mkoani Arusha.Mulongo
aliyasema hayo juzi alipokuwa akiahirisha kikao cha Kamati ya Ushauri
ya Mkoa (RCC), na kusisitiza kuwa serikali haitaki kuona wananchi
wasiokuwa na hatia wakipoteza maisha kutokana na matukio ya wachache
ambao wanataka kuvuruga amani na utulivu.Alisema kuwa matukio hayo
haelewi ni kwa nini mkoa wa Arusha na Zanzibar zinalengwa kwa mabomu
na kueleza kuwa wapo watu ambao wanatengeneza kizazi ambacho hakitaki
amani.Akawataka wananchi wasikalie taarifa za kuwepo watu wenye
mabomu, bali waisaidie serikali kuwafichua kwa sababu wapo miongoni
mwa jamii wanayoishi nao."Leo angalia matokeo yake, wanaofanya
matukio haya wanatoka wapi kama sio miongoni mwetu, kila kiongozi
aliapa kuilinda amani na wananchi hivyo timizeni wajibu wenu ili
wahusika wanaofanya haya waweze kuchukuliwa hatua,''alisema.Tangu
mwaka huu kuanza kumetokea zaidi ya matukio matatuya bomu mkoani
Arusha, yakiwemoya Aprili ambapo watu kadhaa walijeruhiwa na mmoja
Sudi Ramadhan alipoteza maisha baada ya bomu kurushwa kwenye baa ya
Night Park iliyopo Mianzini.Pia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan,
Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Taasisi ya Kiislamu ya Answar
Muslim Youth centre, Shehe Soud Ally Soud alijeruhiwa kwa bomu akiwa
na mgeni wake kutoka Kenya, Shehe Muhaji Hussein Kifea wakati wakila
daku nyumbani kwake eneo la Majengo. Kifea amevunjwa miguu yote miwili
na kupoteza vidole vitatu vya mguu wa kulia.Pia watu wengine wanne
wenye asili ya Asia wamejeruhiwa kwa bomu akiwemo mmoja aliyepoteza
mguu wakati bomu lilipovurumushwa kwenye mgahawa wa Vama Traditional
Indian Cuisine.Akizungumzia ziara ya Mwenyekiti huyo wa SARPCCO, Mangu
alisema Ndeitunga yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kwa ajili ya
kuangalia utekelezaji wa maazimio ya nchi za ukanda huo, kuhusu
kukabiliana na uhalifu wa mipakani kama usafirishaji dawa za kulevya,
wizi wa magari, ugaidi na mwingineo.Akizungumzia mafanikio yake akiwa
Mwenyekiti wa ukanda huo, Ndeitunga alisema hana shaka ya kuwa
Tanzania itakuwa imetekeleza vema udhibiti wa uhalifu
mipakani.Ndeitunga alisema katika ukanda huo wanasisitiza usawa wa
kijinsia katika ngazi za maamuzi za polisi ambapo lengo ni kufikia
asilimia 50 kwa asilimia 50, jambo ambalo linachukua muda huku kila
nchi ikitakiwa kusimamia malengo hayo.Lakini alisema katika
kuhakikisha wanafanikiwa kudhibiti uhalifu katika ukanda huo, Polisi
ni wachache na hawako kila sehemu lakini wananchi wa nchi zote wako
kila mahali na rahisi kusaidia polisi kudhibiti hali hiyo."Tatizo
kubwa katika ukanda huu nidawa za kulevya kwa mabara mengine kuingiza
dawa kwetu, hivyo tunahitaji msaada wa kifedha ili kukabiliana na
biashara hii ili kutuwezesha katika upelelezi, mafunzo na vifaa huku
viongozi wa dini, mila, siasa na wengineo kuhamasisha jamii kuhusu
madhara ya dawa hizo kama ukimwi,"alisema.Alisema changamoto kubwa
inatokana na ukosefu wa vifaa vya kutambua dawa hizo, mafunzo kwa
polisi pamoja na msaada wa jamii ya kila nchi na kucha kuwa
wasikilizaji wa tatizo.Alisema katika uongozi wake wamefanikiwa katika
operesheni kubwa iliyojulikana kama Operesheni Usalama ambayo
ilijumuisha umoja wa SARPCCO na ule wa Afrika Mashariki EAPCCO,
operesheni ambayo ilileta manufaa makubwa katika kukabiliana na
uhalifu unaovuka mipaka huku akiwa na malengo ya kuendesha operesheni
na ukanda mwingine.Ndeitunga aliyepokea uenyekiti wake kutoka
Tanzania, baada ya kumaliza ziara nchini ataelekea Malawi kwa ajili
ya utekelezaji wa kazi hiyo na Septemba mwaka huu atamaliza uenyekiti
wake na kuukabidhi kwa mkuu wa Polisi nchini Lesotho. 

0 comments:

Post a Comment