Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza
umeendelea kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa
na unene zaidi eneo la mapajani, katika makalio na katika mahips ni
vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya.
Wataalamu wanasema kuwa, mafuta
yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya ambazo
huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe.
Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makalio makubwa ni bora kuliko
mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo
hayasaidii chochote.
Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la
Kimataifa la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya
kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine katika siku zijazo
madaktari watatakiwa kuangalia njia za kuyahamisha mafuta mwilini na
kuyapalekea katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu kutokana na
magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa mengineyo kama kisukari.
Watafiti hao wameeleza kwamba, kuwa na mafuta kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo makubwa ya umetaboli.
Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba,
ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za
nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno.
Ingawa suala hilo linaonekama kana kama
ni kinyume, lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko kuna faida kwani,
wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi hutoa mada inayoitwa cytokines
ambayo huleta uvimbe katika mwili.Mada za cytokines zinahusiana moja kwa
moja na magonjwa ya moyo na kisukari. Kuyeyuka taratibu kwa mafuta
katika mapaja pia husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa wingi
na husaidia kudhibiti sukari katika damu na jinsi mafuta
yanavyochomeka.
Dakta Konstantinos Manolopoulos
aliyeongoza utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la
muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na kwamba unene wa mahips
na mapaja ni mzuri kuliko unene wa tumbo.
0 comments:
Post a Comment