Sista
wa kanisa katoliki jimbo la Mtwara sista Sophia Nampwapwa amefariki
dunia kwenye ajali mbaya ya barabarani, baada ya gari alilokisafiria
kuacha njia na kupinduka mara 2 kwenye barabara ya chuno katika manispaa
ya Mtwara/Mikindani.
Sista
Sophia amefariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Mtwara ya Ligula, na miongoni mwa viongozi waliostushwa na ajali
hiyo na kufika hospitalini hapo kufuatilia, ni askofu wa jimbo la
Mtwara Gabriel Mmole.
Kamanda
wa polisi mkoa Mtwara kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Augustine
Ollomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 11 jioni,
ikihusisha gari aina ya land rover lenye usajili namba T 589 AAG na
kuongeza, polisi inamshikilia dreva wa gari hilo aliyetambulika kuwa
Godwin, kwa uchunguzi zaidi.
Hata
hivyo baadhi ya walioshuhudia ajali hiyo wamesema, imetokea wakati
dreva alipokuwa akijaribu kumkwepa mpanda baskeli aliyekatisha ghafla
barabarani huku dreva huyo akidaiwa, alikuwa kwenye mwendo kasi.
Akizungumzia
kifo cha sista Sophia Nampwapwa kaimu mama mkuu shirika la masista wa
mkombozi Mtwara sista Veronica amesema, wamepokea kwa mstuko mkubwa kifo
hicho lakini wanawashukuru wote waliojaribu kuokoa maisha yake ikiwa ni
pamoja waliombeba na kumwaisha hospitalini pamoja na madaktari.
0 comments:
Post a Comment