Timu
ya taifa ya Arggentina imepokelewa kwa shangwe na maelfu ya watu
waliotaka kuwapongeza wachezaji wao, kuanzia uwanja wa ndege. Wanandinga
hao walishuka kutoka kwenye ndege maalum iliyokuwa imenakshiwa kwa
rangi za timu hiyo ikiwa na maandishi yaliyomaanisha 'Asante Argentina'
kwa lugha ya kwao.
Wachezaji hao walipita kwenye mitaa wakiwa ndani ya mabasi maalum huku kukiwa na mapokezi makubwa kuwahi kushuhudiwa.
Argentina
iliingia fainali za kombe la Dunia 2014, na kushindwa kutimiza ndoto
yao ya kutwaa kombe hilo kwa kufungwa na timu ya Ujerumani kwa bao moja.
Rais wa
Argentina Cristina Fernandez de Kirchner (kulia) akimsalimia mchezaji
Lionel Messi mara baada ya kuwapokea leo baada ya kurudi nchini kwao.
Mchezaji
wa Argentina Lionel Messi Julai 13, 2014 amepokelewa nchini kwao na
Rais Cristina Fernandez de Kirchner mara baada ya kushinda zawadi ya
Mpira wa Dhahabu iliyotokana na kuwa mchezaji bowa katika mashindano ya
Kombe la Dunia yaliyomalizika jana nchini Brazili. Mshabiki wengi wa
soka wamempongeza sana mchezaji huyo kwa jinsi alivyocheza japo timu
yake haikuweza kuwashinda Wajerumani.
Rais wa Argentina akimpa pongenzi meneja wa timu yao Alejandro Sabella.Pembeni ni mchezaji Lionel Messi.
Viongozi wa nchi ya Argentina wakifurahia jambo mapema leo mara baada ya kurudi nchini kwao.
0 comments:
Post a Comment