Ndege
ndogo ikiwa imebeba wafanyakazi wa jeshi la Marekani imetua kwa dhalura
katikati ya barabara nchini Uganda baada ya kuishiwa mafuta.
Philip
Mukasa msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda amesema ndege hiyo
iliyokua imebeba abiria wanane wakiwemo wafanyakazi wawili wa ndege
hiyo, ilikuwa iliyokua ikielekea Sudani ya Kusini baada ya rubani
kugundua hakuwa na mafuta ya kutosha aliamua kurudi uwanja wa kimataifa
wa Entebbe ndipo ikabidi itue kwa dhalura katikati ya barabara kwenye
mji wa Mityana uliopo kilomita 67 (maili 41) kutoka mji mkuu wa Kampala.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa, rubani ametua ndege kwa dhalura katikati ya barabara na watu wote wametoka salama.
Haikujulikana
ni kwa nini rubani hakuelekea Sudan ya Kusini na badala yake kaamua
kutua katikati ya barabara baada ya ndege hiyo kuishiwa mafuta.
0 comments:
Post a Comment