Wema Sepetu Amlipua Kajala Kisa UNAFIKI

Wema Isaac Sepetu (25), amemlipua
aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja 'K'
ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki,
habari ambayo ilisambaa katika
mitandao mbalimbali ya kijamii.

Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa
akisema kwamba licha ya watu wengi
kuamini wamepatana, hakuna ukweli
kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia
kutomthamini na kutokuwa karibu naye
kama zamani likiwemo suala la kumsifia
mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala
(Dacutee).
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema
alisema alishangaa kuona Kajala anamwita
mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye
tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma
kama alivyosema.
"Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni
mnafiki 'ok fine' na huo unafiki wangu
unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku
yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa
kuwa yeye ana bifu la kumchukulia
bwana'ke na mimi nijiingize kwenye bifu
lao?
"Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty
Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama
wanavyofanya hao watu wake anaozurura
nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo
hawavijui kiundani wake? Nasema siyo
sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema
Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja
na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama
zamani na yeye halafu kama anamaindi
kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man
ambaye ana uhusiano naye aliweka picha
ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?"
aliwaka Wema.
Akiendelea kutema cheche, Wema alisema
anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli
wa matatizo yao na siyo kusingizia watu
wengine.
"Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu
(waandishi) kuhusiana na tatizo letu, si
nimetoa kinyongo changu ambacho
nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa najiona
mwepesi na kama na yeye anataka
kusafisha moyo wake anatakiwa afunguke,
kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na
kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani
nimechoka na nina mambo mengi ya
kufanya," alisema Wema.
Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala
na kupiga picha za pamoja wakiserebuka
hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile
kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo
maana alivyoombwa apige picha na Kajala,
hakusita kufanya hivyo.
"Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani
na upendo kwa kila mtu, siwezi
nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo
ilivyotokea, niliombwa nipige picha ya
pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na
nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda
zangu kulala," alimalizia kusema Wema.
Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies
liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala
kuwa ametembea na aliyekuwa bwana'ke,
kigogo aliyetajwa kwa jina la CK.
Chanzo: Gpl

0 comments:

Post a Comment